The House of Favourite Newspapers

RC ALLY HAPI AAHIDI MAKUBWA IRINGA

Ally Hapi akiongea jambo katika ofisi za Global Group.

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ali Hapi,  amesema anatarajia kuufanya mkoa wake kuwa wa kitalii na pia kuwa kitovu cha chakula nchini.

Happi akifanyiwa mahojiano na Mhariri, Elvan Stambuli ndani ya studio za Global Tv Online.

Akizungumza na Global TV leo alipotembelea kampuni ya  Global Group, Happi alisema mkoa huo una bahati ya kuwa na hifadhi kubwa ya utalii ya Ruaha lakini haitangazwi ili kuwafanya watalii kwenda kuwaona wanyama huko.

…Akiwa na Meneja Mkuu, Abdallah Mrisho (katikati) na Mkuu wa Global TV, James Range.

“Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ni kubwa sana na ina kila wanyama lakini bado Iringa haijawa sehemu ya utalii. Nitahakikisha watalii wanakuja kwa wingi pale.

…Akipata maelekezo kutoka kwa Range ndani ya studio za Global TV.

“Lakini pia Iringa ni moja ya mikoa inayozalisha mahindi, nitahakikisha kunakuwa na viwanda vingi vya kusaga nafaka ili tuwe tunasambaza unga badala ya mahindi.

 

“Soko lipo kwa sababu Dodoma ambako ndiyo makao makuu ya nchi ni karibu na Iringa kuliko Morogoro na Singida kwani ni zaidi kidogo ya kilomita 200, hivyo tunaweza kutumia ukaribu huo kwa kupata soko la unga lakini pia kwa utalii,” alisema Hapi.

…Akisalimiana na mtangazaji wa Global TV, Judith Mlwale.

Alisema atahakikisha watumishi wa serikali wanafanya kazi ipasavyo badala ya kukaa bila kufanya kazi na atahakikisha wataalamu wa kilimo, afya, elimu na kadhalika wanakuwa karibu na wananchi.

Happi akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Digital, Edwin Lindege.

“Kila mkuu wa idara atatakiwa anionyeshe kazi gani ameifanya kwa wiki, hii itasaidia kuwafanya watoke ofisini na kwenda kwa wananchi,” alisema Happy.

..Akisalimiana na mhariri, Walusanga Ndaki.

Katika ziara hiyo alitembelea vyumba vya habari vya magazeti pendwa ya Uwazi, Risasi, Wikienda, Amani na Ijumaa.  Pia alitembelea chumba cha habari cha magazeti bora ya michezo nchini, Championi na Spoti Xtra  na kile cha Global TV On Line.

…Akisalimiana na mpigapicha wa Global TV, Hillary Daudi.

FUATILIA HAPA Taarifa ya Habari ya Global Tv Online usikie alichokisema Ally Happi

Comments are closed.