The House of Favourite Newspapers

RC Chalamila Aagiza Wananchi Wakamatwe na Kuswekwa Ndani

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwaweka ndani wananchi wote wa Kijiji cha Ngole katika Kata ya Ilungu kwa kuharibu mradi wa maji wa kijiji jirani cha Machesye.

 

Wanakijiji hao wanadaiwa kuvamia na kuharibu mradi huo kwa kuvunja banio na kukata mabomba yaliyowekwa kuanzia kwenye chanzo cha maji hadi kwenye makazi ya kijiji hicho cha jirani.

 

Chalamila alitoa agizo hilo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya waliokaa kupokea na kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mashesye, Osiah Mwakalila, aliwasilisha taarifa juu ya uharibifu waliofanyiwa na majirani zao, akidai kuwa pia walikuwa wanatishia kuwashambulia endapo wangewazuia kutekeleza uamuzi wao.

 

Aidha, Mwakalila alisema mradi huo ambao ulibuniwa na wananchi wa kijiji chake na kugharimu Tsh. Milioni 27, ungekamilika jana.

Comments are closed.