The House of Favourite Newspapers

RC Chalamila: Matangazo ya Vifo Mtaani, Tabia Hiyo Ife

0

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amepiga marufuku kufanyika kwa shughuli za mazishi kwa kutumia magari ya matangazo ya vifo mitaani, ambayo yamekuwa yakianzia mochwari mpaka nyumbani kwa marehemu kitu ambacho kimelalamikiwa kuleta usumbufu kwa wakazi wa Mkoa huo.

 

“Wananchi wa Mbeya wamekuwa wakipitisha magari ya matangazo mitaani wakati wa misiba huku wakitaja wasifu wa Marehemu, picha ya Marehemu ikiwa mbele ya gari na msafara ukifuata, hii imetajwa kuwasumbua wengine, ninaagiza kuanzia Februari 24, 2021, tabia hiyo ikome,” RC Chalamila.

Leave A Reply