The House of Favourite Newspapers

RC HAPI: Hata Msigwa Anaweza Kurudi CCM – Video

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ally Salum Hapi, leo Alhamisi, Agosti 30, 2018 ametembelea ofisi za makampuni ya Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam kisha kuzungumza na viongozi na wafanyakazi wa makampuni hiyo.

 

Akizungumza na Global TV, RC Hapi, amesema hakuna ugomvi wowote wa kisiasa kati yake na viongozi wake wa chini wakiwemo wakuu wa wilaya, Madiwani pamoja na wabunge wa mkoa wake.

 

RC Hapi ameongeza kuwa kikubwa anachokifanya Iringa ni kupambana na shida za wananchi wake na yuko tayari kushirikiana na wasaidizi wake hata kama ni wa vyama pinzani kama vile Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa ambaye akiona maendeleo yanapamba moto anaweza kuamua kurudi nyumbani yaani CCM.

MSIKIE ALLY HAPPI AKIFUNGUKA HAPA

Comments are closed.