The House of Favourite Newspapers

RC KUNDENGE AFANYA ZIARA YA KUTATUA KERO ZA WANANCHI PUGU.

0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amefanya ziara ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi Pugu Stesheni ambapo ameahidi kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hao.

Akizungumza wakati wa Ziara hiyo Kunenge amesema kuwa changamoto alizozipokea atahikikisha zinapatiwa ufumbuzi wa haraka.
“Nimepokea changamoto zenu ikiwemo za elimu, miundombinu, maji, umeme, afya, migogoro mbalimbali na changamoto za kisheria wanasheria watazishughulia na nyingine naagiza watendaji kuhakikisha wanazishughulikia Mara moja.

Pia amepokea Malalamiko ya Wananchi kuhusu kupatikana kwa kulasimishwa kwa ardhi ambayo yamekuja kuanzia Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willlium Lukuvi, kutoa maelekezo kwa watendaji wake kwanza maeneo hayo yalasimishwe haraka,” alisema Kunenge

“Tuliambiwa tutoe shilingi laki 1 na nusu, kwa ajili ya kulasimishiwa adhi zetu lakini tunashangaa tunaambiwa tulipe tena laki 170000 hii si sawa”walisema Wananchi

Pamoja na hayo Mkuu wa Mkoa, Kunenge, aliwataka watendaji kushugulikia kero hiyo kwa haraka.
Kwenye ziara hiyo RC Kunenge aliambatana na watendaji mbalimbali wa Mkoa akiwemo katibu tawala wa Mkoa, wakuu wa idara pamoja na viongozi wa Wilaya ya Ilala.

Leave A Reply