The House of Favourite Newspapers

RC KUNENGE AWATAKA WANANCHI KUCHUKUWA TAHADHARI DHIDI YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.

0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewataka wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya mvua zinazoendelea kunyesha kwa kuhakikisha wanafuatilia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya hewa TMA ili kujikinga na athari za Mafuriko.

RC Kunenge amewaelekeza TARURA, TANROAD, DAWASA, REA na TANESCO kuhakikisha wanaendelea kukarabati na kurejesha miundombinu yote iliyoathiriwa na mvua ikiwemo ili huduma ziweze kurejea Kama awali.

Aidha RC Kunenge ametoa pole kufuatia vifo vya watu 12 vilivyojitokeza kutokana na mvua ya juzi ambapo amesema mbali na vifo hivyo pia zaidi ya nyumba 800 ziliathiriwa na mvua na kusababisha kero kwa wananchi.

Pamoja na hayo RC Kunenge ameeleza kuwa Kamati za maafa na vikosi vyote vinaendelea kuzunguka maeneo mbalimbali ya jiji hilo ili kukabiliana na madhara yoyote yanayoweza kutokea.

Hata hivyo RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kutupa taka kwenye mito na Mifereji kwakuwa ndio chanzo Cha mitaro kuziba na kusababisha Mafuriko.

Leave A Reply