The House of Favourite Newspapers

RC Makalla Azindua Soko la Coca Cola Kwanza Kimbilio la Wamachinga na Mama Lishe

0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla (mwenye suti) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa soko hilo.

 

 

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla leo amezindua ujenzi wa soko jipya la kisasa linalotarajiwa kujengwa na Kampuni ya Coca Cola Kwanza eneo Dampo ya zamani Kigogo jijini, ambalo linatarajiwa kuwa kimbilio la wafanyabiashara wadogo wakiwemo mama lishe na wamachinga walioondolewa sehemu barabarani.

Amos Makalla (kushoto) akizindua jiwe la msingi kwenye soko hilo, kulia ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge.

 

 

Akizungumzia kwenye uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ameipongeza kampuni ya Coca Cola Kwanza kwa kushirikiana na serikali katika harakati za kimaendeleo.Amesema RC Makalla kuwa soko hilo la kisasa kabisa linatarajiwa kuwa na uwezo wa kuchukua watu 100.

RC Makalla akizungumza baada ya uzinduzi huo.

 

 

RC Makalla ameipongeza kampuni hiyo kwa kufanya kitendo hicho cha kurudisha fadhila kwa wateja wake na wananchi kwa ujumla na kuwaomba wananchi waendelee kuiunga mkono kampuni kutokana na uzalendo wake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Kwanza, Unguu Sulay akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) baada ya uzinduzi huo.

 

 

“Naomba niipongeze kampuni hii kwa uzalendo wake wa kurudisha fadhila kwa wateja wake na wananchi kwa ujumla na nitumie nafasi hii kuziomba na taasisi zingine nazo kufanya uzalendo kama huu ili tulijenge taifa letu” alimaliza kusema RC Makalla.

 

 

Akizungumza baada ya uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Coca Cola Kwanza, Unguu Sulay amesema lengo la kampuni hiyo imeamua kuwekeza kwenye mradi huo ili kurejesha fadhila kwa wateja wake na wananchi haswa vijana na kinamama lishe.

 

 

Mkurugenzi huyo amesema katika kuhakikisha wanalinda mazingira sokoni hapo wataweka kituo cha kupokea taka za plastiki ambazo watazitumia kutengeneza bidhaa zingine.

 

 

Unguu alimalizia kwa kuwaomba wananchi waendelee kuiunga mkono kampuni hiyo kongwe yenye miaka 135 na yenye malengo ya kufika mbali zaidi na kutoa huduma bora zaidi kwa wadau wake ambao ni wananchi.

Leave A Reply