The House of Favourite Newspapers

RC Makonda aendelea na Ziara ya kukabidhi miradi

0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameendeleea na ziara ya kukabidhi miradi kwa kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi katika Wilaya ya Kinondoni. Akizungumza na Global Publishers, wakati wa Ziara Hiyo Rc.Makonda alisema kuwa Wilaya ya Kinondoni imekuwa ni mfano wa kuiga na Wilaya nyingine kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kutumia vyanzo vya mapato ya ndani, Serikali kuu pamoja na wadau kama ilivyotekelezwa katika Manispaa ya Kinondoni

“Kila Halmashauri katika Mkoa wa Dar es Salaam inakusanya mapato hivyo zinapaswa kutekeleza miradi ambayo itacha alama kama ambavyo Manispaa ya Kinondoni imeweka alama katika miradi mikubwa ya Maendeleo chini ya Serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli pamoja na usimamizi mzuri wa Mkurugenzi mzalendo Ndg. Aron Kagurumjuli.


“Kinondoni nawapongeza sana, mmefanya kazi inayoonekana nakuacha alama kwa Wananchi, kipindi cha nyuma haya mambo hayakuwepo licha ya kwamba Manispaa zilikuwa zinakusanya mapato lakini katika uongozi wa miaka mitano ya Dk. Magufuli mmeitendea haki ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ” amesema Makonda.

Aidha Rc.Makonda amekabidhi mradi wa Soko la kisasa la Magomeni,Soko hilo ambalo limejengwa kwa fedha kutoka Serikali kuu, ni chanzo kikubwa cha mapato katika Manispaa ya Kinondoni litakaloongeza hadhi ya wafanyabishara watakaoendesha shughuli zao bila kubugudhiwa.


Katika Ziara hiyo Mhe. Makonda ametembelea miradi mingine ikiwemo, ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Shekilango hadi Bamaga ,Uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu Mwenge pamoja na Stedi ya daladala iliyopo Mwenge.
Kesho Jumatano RC Makonda ataendelea na ziara yake kwenye Jimbo la Kibamba ambapo atakabidhi miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Chama cha Mapinduzi CCM.

Leave A Reply