The House of Favourite Newspapers

RC MAKONDA AMPA MILIONI 5 MAMA WA GODZILLA

RC Paul Makonda akimbeba mtoto wa Marehemu Godzilla wakati akitoa pole kwa familia ya marehemu.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema atampa pesa kiasi cha Tsh milioni tano, mama mzazi wa aliyekuwa Rapa wa Bongo, marehemu Golden Jacob Mbunda ‘Godzilla’ ili zimsaidie katika kuwatunza watoto wa marehemu.

Makonda amesema hayo leo Jumamosi, Februari 16, 2019 katika Uwanja wa Salasala wakati akitoa salam za pole kwa familia, ndugu na wasanii kwa kuondokea na msanii huyo aliyeaga dunia usiku wa kuamkia Februari 13, mwaka huu.

“Ndugu yetu alikuwa na mipango wa kumsaidia mama yake kiuchumi, akawa amempa milioni nne lakini akawa na malengo ya kumpa milioni tano  ili aweze kuanzisha famasi kama sehemu ya kujitengemea kiuchumi.
“Nitampa mama mzazi wa marehemu Godzilla kiasi cha shilingi milioni tano, nitampa Fid Q azilete kwa Mama Jumatano ili zimsaidie kuwatunza wajukuu na kufanya kile alichopanga baada ya kutumia pesa nyingi katika atibabu ya Godzilla,” amesema Makonda.

Mwili wa Zilla utazikwa leo katika Makaburi ya Kinondi jijini Dar es Salaam.

Mwili wa GODZILLA UKiagwa SALASALA Muda Huu

Comments are closed.