The House of Favourite Newspapers

RC MAKONDA, APOKEA TSH MIL.50 KUTOKA KWA PBZ

0

BENKI ya watu wa Zanzibar [PBZ], imemkabidhi hundi ya Tsh Mil.50, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya changia ujenzi wa ofisi za walimu aliyoianziasha katika mkoa wake.

RC Makonda Akikabidhiwa Hundi ya Tsh Mil.50

RC Makonda ambaye amefanya ziara ya siku moja, katika mkoa wa mjini Magharib, Zanzibar kwa dhumuni la kutembelea vivutio mbalimbali na maeneo ya kihistoria yaliyopo katika kisiwa hicho, pia kuimarisha uhusiano wake mzuri wa kikazi na mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud, ambapo alifanikiwa kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo katika Benki iliyomkabidhi hundi.

RC Makonda Katika Picha ya Pamoja na RC Ayoub na Wanafunzi

Aidha RC Makonda alitembelea katika Pango la Tumekuja lililojengwa enzi za utawala wa, Sultan Said Said Barghash kwa ajili ya kusafirishia watumwa.
Alitembelea makumbusho ya jengo ambalo lilikuwa likitumika kuuzia watumwa enzi za Ukoloni ambalo lilifungwa rasmi mwaka 1873 na sasa eneo hilo linatumika kama kanisa “Kanisa la Mkunazini” mbali na kutumika kama sehemu ya Historia visiwani humo.

RC Makonda Akizungumza Jambo na RC wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mahmoud

Alifika pia eneo la Mtoni Marine, inakojengwa hoteli kubwa Afrika Mashariki ambayo iko mjini na yenye uwezo wa kupokea wageni wakiwa na Meli zao 12, pamoja na eneo la darajani unapofanyika ukarabati wa Jumba la treni ambalo limo kwenye orodha ya urithi wa dunia.

Hoteli ya Kifahari Iliyopo Eneo la Mtoni Marine

Alihitimisha ziara hiyo kwenye shamba la Viungo la ‘Spice Farm’ la Kizimbani lenye viungo vya chakula na mboga mboga ikiwemo Tangawizi, Binzari, Pilipili Manga, Karafuu, mdalasini, Hiliki, mchaichai na kadhalika.

RC Makonda Akionyeshwa Baadhi ya Viungo, Katika Shamba la Spice Farm

NA ISRI MOHAMED/GPL

 

Leave A Reply