The House of Favourite Newspapers

RC Malima awataka wanahabari Morogoro kuwa Mabalozi wa Utalii

0

Mkuu wa Mkoa Morogoro Adam Malima amewataka wanahabari mkoani humo kuwa mabalozi wa utali Kwa kuandika Habari na makala mbalimbali zitakazowavuta watalii wengi kutoka nje na ndani ya nchi

Rc Malima ameyasema hayo wakati akifungua Mafunzo kwa wanahabari  zaidi ya 30 yaliyoandaliwa na  Chama Cha Wafanyakazi WA Vyombo vya Habari (TAMPA) kwa kushirikiana na TANAPA  akisema Mkoa wa Morogoro unahifadhi Tatu Kubwa ambazo ni Mikumi,Udzungwa na Mwalimu Nyerer

Rc Malima amesema bado hamasa ni dogo Kwa wanahabari Kuhusu uandishi wa Habari za utalii  na Mazingira   hivyo akaahidi kugharamia wanahabari waliohidhiria mafunzo hayo kuzunguka katika hifadhi hizo  kuona vivutio vilivyopo na kuvitangaza

“Nataka timu ya Waandishi wa Habari  40  tukafanye utalii , tulale Mikumi kisha twende Udzungwa na badae Mto Kilombero tukitoka hapo nataka Morogoro iwe namba moja Kwa utalii nchin

Aidha Malima amesema serikali ina mpango kufungua geti lingine kupitia Kilosa kuingia Hifadhi ya mikumi  kutokana na kuwepo Kwa treni ya mwendokasi Ili  kurahisisha shughuli za utalii  katika hifadhi hiyo ambapo kwa Sasa wanalazimika kusafiri zaidi ya kilometa 100 kutoka kilosa Hadi Mikum

Anasema hifadhi ya Mikumi inafikika kwa njia  kadhaa ambazo ni barabara ya TAZAM, Reli ya kati na Reli ya SGR na njia ya anga  hivyo watalii wanapata fursa ya kuona wanyama kirahis

Pamoja na hayo amewataka wadau mbalimbali  kuanza kujenga hoteli nzuri zenye viwango  katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kisaki Ili kuhudumia watalii wanaotembelea hifadhi ya Mwalimu Nyerere, Mikumi, Doma Kwa hifadhi ya Mikumi na Ruaha kwa hifadhi ya Udzungw

Kwa Upande wake  Rais TAMPA, Simon Mkina amesema lengo la semina hiyo ni kuwaandaa wanabari kuwa sehemu ya utalii Kwa kushiriki moja kwa moja Ili kutimiza malengo ya Serikali  kupitia filamu ya THE ROYAL TOU

“Tumeanzia Dar es Salam na leo tupo Morogoro  tunatoa mafunzo haya Kwa kushirikiana na wakufunzi kutoka Chuo Cha Taifa cha Utalii Ili kupata mabalozi wazuri masula ya utalii na watal

Naye amesema mwaka 2023 jumla ya watalii Milioni 1.8 kutoka Mili. 1.3 mwaka 2022 na hii ingezeko.kubwa baada ya filamu ya THE ROYAL TOUR  ambayo imekua chahu kubwa kwa nch

Naye katibu wa chama wa Waandishi wa Habari mkoa Morogoro (MORO PC) Lilian Kasenene  ameshukuru kwa niaba ya waandishi wa habari Morogoro Kwa kupata mafunzo hayo ambayo yamewajenga wanahabari kuwa na utayari wa kuripoti masuala ya utalii.

Leave A Reply