The House of Favourite Newspapers
gunners X

REKODI MBILI MPYA…Ni Simba vs Yanga Cecafa

BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), wakishirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana limezindua rasmi mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame) yanayotarajiwa kuanza Juni 29, mwaka huu huku Simba na Yanga zikipangwa kwenye kundi moja.

 

Hii ni rekodi mpya kwa michuano yote ambayo imekuwa ikiandaliwa kwenye ukanda huu ambapo hakuna kipindi huku nyuma ambacho timu hizo zimewahi kuwekwa kundi moja.

 

Hata hivyo, pamoja na kwamba timu hizo zimepangwa kundi moja, kuna uwezekano mkubwa zikakutana tena kwenye hatua za mbele aidha fainali au mshindi wa tatu kama zote zi­tapenya hali ambayo inaonye­sha kuwa kuna uwezekano timu hizo zikavaana mara mbili ndani ya mwezi mmoja jambo ambalo pia ni rekodi.

Katika mashindano hayo yatakayoshirikisha timu 12 ambapo Kundi A kuna Azam ya Tanzania, Resps (Uganda), JKU (Zanzibar), Kator (Sudani ya Kusini) na Kund B, Rayon Sport (Rwanda), Gor Mahia (Kenya), Lydia Ludic (Burundi) na Ports Djibouti wakati Kundi C kuna Simba, Yanga zote za Tanzania, St George kutoka Ethiopia na Dakadaha ya Somalia.

Akizungumza katika uzin­duzi huo, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye, alisema kuwa kwa upande wao wana furaha kubwa mashindano hayo kufanyika tena hapa nchini baada ya kupitia miaka miwili iliyokuwa na changamoto nyingi huku akiwatambulisha Azam TV, kama wadhamini wa mashindano hayo.

 

“Kwetu kama baraza tuki­shirikiana na TFF ni jambo la fu­raha kuona mashindano haya tunaweza kufanya tena hapa nchini kwa sababu imani yetu ni kuona yanaendelea kuwa endelevu kwa miaka inayokuja lazima nchi zijipange kuandaa kutokana na kupata wad­hamini wapya ambao ni Azam TV watakaokuwa wakirusha mashindano hayo.

 

“Suala la zawadi bado lipo vilevile kama ilivyokuwa kwa sababu bado tunapata kutoka kwa rais wa Rwanda, Paul Kagame tangu kuanza kwa mashindano haya lakini kwa nini Simba, Yanga zimekuwa katika kundi moja? Ni kwamba Azam wao ni mabingwa wa­tetezi wa kombe hili, Yanga ni mabingwa wa nchi msimu uli­opita isipokuwa Simba imeingia kupitia nafasi ya upendeleo kwa nchi muandaaji na kuwa kundi moja na Yanga, imetoka­na tu katika kupanga ratiba kutokana na ushiriki wake,” alisema Musonye.

 

Katika hatua nyingine, bingwa wa michuano hiyo atap­ata zawadi za Dola za Marekani 30,000 (Sh milioni 60), mshindi wa pili Dola za Marekani 20,000 (Sh milioni 40) na mshindi wa tatu Dola za Marekani 10,000 (Sh milioni 20).

 

Mara baada ya ratiba hiyo msemaji wa Simba, Haji Man­ara kupitia mtandao wa Kijamii wa Instagram aliandika kuwa: “Kwa jinsi walivyo taabani si tutawapiga sita ? au na hii wa­taumwaga kama walivyokimbia kwenye Sport Pesa Supar Cup?”

Stori na Ibrahim Mussa, Dar es Salaam

Comments are closed.