The House of Favourite Newspapers

Rekodi za Ronaldo Zatikisa

0

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ameendelea kuweka rekodi licha ya umri wake kuonekana kumtupa mkono baada  ya jana kuwa mchezaji mwenye magoli mengi kwenye michuano ya Euro akiwa na magoli 11  akipachika  magoli mawili kwenye mchezo dhidi ya Hungary walioshinda kwa magili 3-0.

 

Ronaldo amefikisha magoli 11 na kumpiku gwiji wa  Ufaransa, Michael Platini aliyekuwa na mabao 9 hivyo kumfanya  kuwa mchezaji pekee mwenye mabao mengi tokea kuanzishwa kwa michuano ya Uefa Euros miaka 60 iliyopita.

 

Rekodi nyingine ni ile ya kucheza michuano hiyo kwa awamu 5(2004, 2008, 2012, 2016 na mwaka huu 2021) na kumpiku Lothar Matthaus wa Ujerumani aliyecheza EUROS awamu 4 (1980, 1984, 1988 na 2000).

 

Aidha mshindi huyo mara 5 ndiye mchezaji pekee kucheza michezo mingi, michezo 22 kwenye michuano ya UEFA EUROS na kuvunja rekodi aliyekuwa anaishikilia kiungo  wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, Bastian Shweinsteiger aliyekuwa amecheza michezo 21.

Mpaka sasa Mreno huyo amefikisha jumla ya mabao 105 mabao 4 nyuma ya Ali Daei wa timu ya taifa ya Iran ambaye anaongoza kuwa mfungaji bora wa muda wote kwa upande wa timu za taifa, rekodi ambayo anazidi kuifukuzia.

 

Baada ya rekodi hizo, Ureno sasa ni kinara wa kundi D akiwa na alama 3 na mabao 3, Ufaransa anashika nafasi ya pili akiwa na alama 3 lakini na bao 1 baada ya kumfunga ujerumani 1-0 hivyo Ureno anaongoza kwa utofauti wa mabao ya kufunga.

 

Michuano hiyo inatazamiwa kuendelea tena usiku wa leo Juni 16, 2021 kunako kundi F, wanaoshika mkia kundi hilo, Uturuki itacheza na Wales waliopo nafasi ya tatu saa 1:00 usiku na kinara, Italia itacheza na Uswizi anayeshika nafasi ya pili saa 4:00 usiku.

Leave A Reply