The House of Favourite Newspapers

Ripoti ya CAG Yabaini Ubadhilifu Mkubwa wa Fedha Mamlaka ya Bandari

0
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere akitoa ripoti mbele ya Waandishi wa Habari

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ametoa ripoti yake ya ukaguzi wa hesabu za serikali mbele ya waandishi wa habari ambapo amebaini mapungufu katika sekta mbalimbali.

 

Moja ya sekta ambayo imekumbwa na mapungufu ni Mamlaka ya Bandari ambapo CAG amesema kumekuwa na ubadhilifu katika Mamlaka ya Bandari kwani kuanzia Januari Mosi 2015 hadi Machi 30, 2020.

       CAG Charles Kichere

Ukaguzi wake unaonesha Mamlaka ya Bandari ilitumia Hundi 7888 zenye thamani ya Bilioni 31.76 kwa ajili ya matumizi ya Mamlaka ya Bandari ambapo pesa hizo zilitolewa kwenye akaunti ya jijini Mwanza, huku Hundi 4777 zenye thamani ya shilingi bilioni 19.41 pekee ndizo zilizowasilishwa kwa ajili ya ukaguzi.

Leave A Reply