The House of Favourite Newspapers

RIYAMA NA STERIO NI KUFA NA KUZIKANA

MWANAMAMA mwenye sifa zote awepo mbele ya kamera za Bongo Movies, Riyama Ally anamuomba Mungu yeye na mumewe, Leo Mysterio waishi miaka mingi ili kila mmoja aje kumzika mwenzake wafikapo uzeeni.

 

Riyama aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, siyo watu wote wanapenda kuombeana dua waishi miaka mingi kama mke na mume, bali huwa wanahesabu tu siku za kuachana, lakini kwa upande wake yeye ni tofauti.

 

“Kila siku ninaomba dua ili mimi na mume wangu tuishi miaka mingi kwa kuziepuka husda za watu ambazo zipo kila kona,” alisema Riyama ambaye ni mkali wa kuigiza sinema za majonzi.

Stori: Imelda Mtema, Dar

ALICHOFANYIWA BAUNSA WA DIAMOND, HATOSAHAU

Comments are closed.