The House of Favourite Newspapers

ROMA AGAWA MAGAZETI YA GLOBAL, KUPIGA SHOO DAR LIVE J2

Roma Mkatoliki

Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoliki juzi Jumatano alihamsha shangwe za kutosha kwa mashabiki wake baada ya kufanya sapraiz ya kuuza Magazeti ya Global Publishers maeneo mbalimbali jijini Dar yakiwemo Mbagala Zakhem, Rangi Tatu, Stendi ya Kibiti na kumalizia Dar Live.

Roma ambaye kutokana na umaarufu wake ilibidi azingirwe na mabaunsa waliokuwa wakihakikisha msanii huyo kipenzi cha wanaburudani afanye kazi hiyo akiwa salama. Magazeti aliyokuwa akiyauza rapa huyo ilikuwa ni Risasi Jumatano na Championi la Jumatano ambayo yaligombewa na umati wa wasomaji walikuwa na shauku ya kumuona.

Sambamba na kuuza magazeti hayo msanii huyo aliwagawia zawadi mbalimbali wasomaji hao ikiwemo fulana za shindano linaloendelea la Tusua Maisha na Global ambalo mshindi hupatikana kila wiki na kujishindia pikipiki, seti ya vyombo na jezi.

Katika tukio hilo wasomaji hao walimpongeza msanii huyo kwa kujichanganya na raia wa kawaida yaani wenye kipato cha kawaida na kipato cha chini ambao wengi waliacha kazi zao na kuungana naye. Maelezo zaidi ya kujishindia zawadi ya pikipiki na nyingine nyingi soma ukurasa wa pili kwenye kuponi.

PICHA: RICHARD BUKOS

 

Comments are closed.