The House of Favourite Newspapers

ROMA KUGAWA ZAWADI MITAANI MBAGALA LEO

Related image

HUKU mwanamuziki anayekimbiza kwenye gemu la Hip Hop Bongo, Ibrahimu Musa ‘Roma Mkatoliki’, akitarajiwa kupiga shoo ya nguvu Jumapili hii kwenye Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, leo (Jumatano) atakuwa anagawa magazeti kwa wakazi wa mbagala bure.

R.O.M.A, atapita kwenye mitaa mbalimbali ya Mbagala akigawa Magazeti ya Risasi Mchanganyiko pamoja na Championi Jumatano, ambayo yatakuwa na kuponi ya Jipatie Pikipiki.

Hata hivyo, kuhusu Jumapili, mkali huyo wa ngoma ya Zimbabwe, ataamsha popo pamoja na Juma Nature kwenye tamasha ba’b kubwa la bure la kuwashukuru Watanzania lijulikanalo kama Tusua Maisha na Global.

Akizungumza na Risasi Vibes, Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho amesema lengo kubwa la kuandaa tamasha hilo litakaloanza kuanzia saa 2:00 Asubuhi hadi saa 12:00 jioni kwanza ni kurudisha fadhila kwa wasomaji wa Magazeti ya Global Publishers ambayo ni Championi, Uwazi, Risasi, Ijumaa Wikienda, Ijumaa, Amani na Spoti Xtra.

“Tunarudisha fadhila kwa wasomaji wetu ambao wamekuwa wakiiunga mkono Global kwa takriban miaka 20 lakini pia kuwaweka karibu wasomaji wetu kwa kutambulisha promosheni kubwa ya pikipiki inayoendelea,” alisema Mrisho.

NI BUREEE

Mrisho alisema kuwa, tamasha hilo litakuwa la bure ambapo wapo wakali kama Juma Nature, Roma Mkatoliki na Man Fongo watakaotoa burudani kwa wote watakaojitokeza.

“Mkongwe Juma Nature tutakuwa naye na atawapagawisha mashabiki kwa kuwapigia nyimbo zake zote kali za zamani na sasa huku naye Roma Mkatoliki akifanya hivyohivyo. Upande wa Singeli tutakuwa na Man Fongo mzee wa Hainaga Ushemeji ambaye naye atawakonga nyoyo wasomaji wote watakaojitokeza,” aliongeza Mrisho.Image result for roma mkatoliki

ZAWADI KIBAO KUTOLEWA

Mrisho anaendelea kuwa, mbali na wasomaji kupata burudani ya bure, watapata kushuhudia washindi wa droo ya pili na tatu wa droo ya Tusua Maisha na Global wakikabidhiwa zawadi zao kama vile pikipiki, headphones za Beats by Dre, seti ya vyombo vya ndani, tisheti na nyingine nyingi.

“Kama ilivyo muendelezo wa kutoa zawadi kila wiki katika droo ya Tusua Maisha na Global, katika tamasha hili tutatoa zawadi nyingi laivu hivyo kama wewe msomaji wa magazeti ya Global hii si ya kukosa huenda ukawa ni wewe utakaye-shinda Pikipiki, tisheti, headphones au dinnerset,” alimaliza Mrisho.

UNAKOSAJE SASA?

Ili kuwa mmoja wa wanafamilia wa Global na kujinyakulia zawadi kibao katika droo ya Tusua Maisha ni simpo sana, wewe nunua tu Gazeti la Championi, Risasi, Uwazi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda au Spoti Xtra kisha funua ukurasa wa pili utakutana na kuponi yenye maelekezo ya namna ya kushiriki. Kumbuka gazeti moja ni kwa msomaji mmoja!

Comments are closed.