The House of Favourite Newspapers

ROMY AFICHUA KILICHOFANYA AMUOE KIJOLI

OFFI­CIAL DJ wa mwana­muziki Nasibu Abdul ‘Dia­mond Platnumz’, Romeo Jones ‘Romy’ ameanika kilichomfanya aingie kwenye maisha ya ndoa na mkewe wa sasa aitwaye Kijoli.  

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Rommy alisema kuwa mkewe huyo alionesha uvumilivu mkubwa enzi za uhusiano wao na ndipo alipobaini kuwa, ndiye mwanamke sahihi wa kumpa heshima ya ndoa.

 

“Niliamua kuoa kwa sababu niliona uvumilivu wa mwanamke huyo kwani nilimfanyia madudu mengi lakini alinivumilia. Kuna wakati nilikua aondoka nyumba na kurudi baada ya siku tatu nikiwa nimelewa lakini alinivumilia, nikabaini huyu ndiye mwenye sifa ya kuwa mke wangu,” alisema Romy.

Comments are closed.