YALIYOJIRI MIAKA 20 YA TWANGA
USIKU wa kuamkia leo Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ imefanya tamasha la kutimiza miaka 20 tangu ianzishwe ambapo umati wa mashabiki na wadau wake walifurika kwenye Viwanja vya Life Club, Mwenge jijini Dar.
Katika tamasha hilo, bendi hiyo ilianza na kutumbuiza kwa nyimbo zake zilizoanza kutamba yangu enzi hizo na mpya. Sambamba na kutumbuiza, ilitolewa historia ya bendi hiyo iliyopitia milima na mabonde mpaka kufikia ilipo sasa.
Matukio katika Picha:
Hivi ndivyo wanamuziki wa bendi hiyo walivyoibukia jukwaani kininja.
Muimbaji wa Twanga, Chalz Baba, akiwajibika.
Mama Mondi (mwanamuziki Diamond) na ‘Anko’ nao walikuwepo.
Kalala Junior (kushoto) na Haji Ramadhani wakishtua ‘kijotijoti’.
Msafiri Diouf (kushoto) akiongoza mashambulizi.
Meneja wa Wasafi Classic Baby (WCB), Bab Tale (kulia) na wasanii wa filamu za Bongo, Steve Nyerere (katikati) na JB wakiwaburudisha mashabiki kwa maneno ya ucheshi.
Wanenguaji wa Twanga wakiwa kazini.
Mwanamuziki mwenye miaka 20 kwenye bendi hiyo, Luiza Nyoni akiimba.
Mashabiki wakijimwaya.
PICHA: RICHARD BUKOS / GPL
Comments are closed.