The House of Favourite Newspapers

Rosa Ree akana kuwa mgumu, hapendi kujibebisha tu!

MWANAMUZIKI wa kike wa miondoko ya Hip Hop Bongo, Rose Robert ‘Rosa Ree’ anayetamba na Wimbo wa ‘One Way’ amesema kuwa watu wengi wanamuona mgumu kutokana na mavazi yake na jinsi alivyo lakini siyo kihivyo bali hapendi kujibebisha kama wafanyavyo wanawake wengine.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Rosa alisema kuna watu wengi wanamuona ana mambo ya kiume kwa sababu hajawahi kuonyesha mpenzi wake hadharani na hiyo ni sababu ya uhusiano wake wa kimapenzi kuwa binafsi zaidi.

 

“Unajua wengi hawanielewi wanasema nina tabia za kiume lakini ukweli sipendi kujibebisha au kujilegeza na pia uhusiano wangu wa kimapenzi ni binafsi zaidi sipendi kuweka hadharani kabisa,” alisema Rosa.

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.