The House of Favourite Newspapers

Rose Ndauka Azindua Jarida Lake

0

1.Msanii wa filamu hapa nchini,Rose Ndauka(kushoto) akizungumza na wanahabari katika hafla hiyo (hawapo pichnai).Kulia kwake ni Meneja wake,RamadhanMwanana. Msanii wa filamu hapa nchini, Rose Ndauka (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)katika hafla hiyo.Kulia kwake ni Meneja wake,Ramadhan Mwanana.

2.Rose Ndauka (kushoto) akifafanua maswali yaliyokuwa yameulizwa na wanahabari (hawapo pichani).Rose Ndauka (kushoto) akijibu maswali yaliyoulizwa na wanahabari (hawapo pichani).

3.Hafla hiyo ya uzinduzi ikiendelea.Hafla hiyo ya uzinduzi ikiendelea.

4.Wanahabari wakichukua tukio hilo.Wanahabari wakichukua tukio hilo.

5.Meneja wa Rose Ndauka, Ramadhan Mwanana (kulia) akitoa ufafanuzi kwa wanahabari.Meneja wa Rose Ndauka, Ramadhan Mwanana (kulia) akitoa ufafanuzi kwa wanahabari.

6.Wakionesha Jarida hilo lililozinduliwa.Wakionesha jarida hilo lililozinduliwa.

7.Mratibu wa shughuli hiyo,Lydia Moyo (kulia) akiwatambulisha wahusika wa tukio hilo kabla ya inshu hiyo kuanza.Mratibu wa shughuli hiyo,Lydia Moyo (kulia) akiwatambulisha wahusika wa tukio hilo kabla ya hafla kuanza.

MSANII wa filamu hapa nchini, Rose Ndauka,leo amezindua jarida lakelinalokwenda kwa jina la ‘ROZZIE MAGAZINE’likiwa na lengo kubwa la kuelimisha na kuburudisha jamii.

Uzinduzi huo umefanyika katika Hoteli ya Double View jijini Dar es Salaam,na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wanahabari.

Akizungumza na wanahabari,Rose amesema kuwa kila mwananchi anayofursa ya kusoma jarida hilokwani linatolewa bila malipo yoyote huku akifafanua kuwa popote linapoweza kupatikana litakuwa ni jambo jema kwa mtu kulichukua na kuweza kulisoma.

Ameongeza kuwa, pia msomaji anaweza kupata ujumbe uliokuwa ndani ya jarida hilo kupitia njia ya mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook,Instragram,Twitter na You Tube huku akisisitiza wananchi kutembelea mitandao hiyo na kuweza kusoma.

Aidha Rose alimalizia kwa kusema, mbali na jarida hilo kuelimisha,kuburudisha na kuikosoa jamii, pia huchochea jamii katika kufanya mambo yatakayowafanya wananchi kufikia malengo yao ya kimaisha ili wajengetaifa lililo bora na lenye maendeleo ambapo jarida hilo litakuwa likitoka kila baada ya mwezi moja.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply