The House of Favourite Newspapers

Rostam, Marioo Wafanya Maangamizi Jukwaa la Tigo Fiesta Arusha

MPANGO mzima wa Tigo Fiesta 2019, ndani ya Uwanja wa Shekhe Amri Abeid jijini Arusha, ulianza
kwa namna hii, ambapo ratiba za wasanii kupanda jukwaani, ilifunguliwa na wasanii wa changa a.k.a Under Ground wa jijini hapo ambao walifuatiwa na Super Nyota waliopatikana ndani ya jiji hilo siku moja kabla ya tamasha hilo kufanyika.

Mbali na hivyo mpango rasmi wa burudani ulianza kwa kufunguliwa na wasanii kutoka nyumba ya kukuzia vipaji ya THT, ambao walifanya ufunguzi huo wa pazia la burudani kwa kucheza nyimbo mbalimbali kisha wakafuatiwa na wababe wa burudani namaanisha kundi la watu wawili la ROSTAM ambalo lipo chini ya Roma na Stamina, waliofungua burudani kwa shangwe za hatari kutoka kwa wapenda burudani wa Chuga huku wakipigwa tafu na Maua Sama ambaye alipanda baada ya kupigwa wimbo wao wa Kibamia alioshirikiana nao kisha Rosa Ree naye akaibuka kama Surprise baada ya wimbo alioshirikiswa na  wakali hao kupigwa .

Kwakuwa tayari kasi ya burudani iliashaanza kupanda chati, mtu wa pili kupanda alikuwa ni mtoto wa Ngarenaro, Dogo Janjaro, ambaye naye ailiibuka jukwaani hapo kwa staili ya pekee akimkaribisha msanii mwenzake kutoka himaya ya Tip Top Connection Maarifa aliyekamua naye kwa shangwe nene kisha kumuachia jukwaa lake na
kuwakaribisha macharii wenzake wa Ngarenaro waliopanda na kuonyesha dansi ya Arusha iliyopokelewa kwa shangwe kubwa kabla ya kuwashusha na kumkaribisha mrembo kutoka pande hizo za Chuga Mimi Mars ambaye kwa namna fulani naye alionyesha uwezo wake wa kucheza na jukwaa kisha akamuachia jukwaa hilo msanii anayekuja kwa kasi katika miondoko ya Rhumba Marioo, ambaye kwa kiasi kikubwa alinogesha jukwaa kiasi cha
mashabiki wote kujikuta wakiduwaa kwa uimbaji wake mkubwa.

Marioo alionyesha maajabu ambayo kiasi fulani yaliwafanya hata waheshimiwa kama Mrisho Gambo, aliyekuwa ndani ya Uwanja huo akipata burudani sambamba na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson kuimba muda wote akipokezana na Catherine Magige pamoja na kuulizia mwanzoni jina la Marioo.

Jukwaa halikutulia kwa burudani kwani baada ya Marioo walipandishwa waheshimiwa hao, kisha jukwaa akaanza kulitawala msanii Country Boy ambaye naye alifanya makamuzi ya aina yake kisha burudani hiyo akikabidhi kwa Young Lunya ambaye alikamua kisawasawa kisha akamuachia jukwaa mrembo wa Arusha Rosa Ree.

Naye alifanya yake kisha akampisha mrembo mwenye sauti ya kumtoa nyoka pangoni, Ruby aliyefanya makamuzi yake kwa live band kama  ilivyokuwa kwa Marioo kisha akaachia jukwaa huru akimpisha Jux aliyefuatiwa na Fid Q aliyetawala jukwaa kwa shangwe kubwa zilizonogeshwa na live band kabla ya kumpisha Barnaba.

Shangwe za burudani hazikupiga nanga kwa wasanii hao tu kwani starehe iliendelea kutawala pande hizo baada ya Maua Sama kupanda kwa mara nyingine akipokea kijiticha Barnaba ambacho naye kimsingi hakuwa mchoyo wa fadhira kwani kabla hajahitimisha wimbo wake wa mwisho alilazimika kutoa surprise ya uhakika kutoka kwa Jay
Mo, ambaye alipagawisha vilivyo na baadaye shoo yake ikakamilika kwa maombi mazuri yaliyofuatiwa na mwimbaji wa nyimbo za Injili, Goodluck Gozibert ambaye naye aliangusha nyimbo zake kadhaa na kuwaachia jukwaa watoto waChuga Weusi.

Kwa namna fulani Weusi walilitendea haki jukwaa kwa nyimbo zao pendwa kwa vijana wa jiji hilo kisha wakahitimisha burudani kwa kumkaribisha One the Incredible aliyemwaga ngoma za Hip Hope kama zotee kisha msanii chipukizi Baddest anayetamba na ngoma yake ya Nikagongee aliyepanda jukwaani hapo na burudani zote kuhitimishwa na vijana wa jiji hilo wanaokwenda kwa jina la Ras Gwandumi.

 

 

Makala; Mussa Mateja.

Comments are closed.