The House of Favourite Newspapers

Rs Berkane Walimwa Faini Kisa Simba

0

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), imetoa adhabu kwa Klabu ya RS Berkane ya Morocco kwa kuvunja sheria za michezo katika mechi mbili za Kombe la Shirikisho ilizocheza dhidi ya Simba, ule wa awali uliochezwa Morocco pamoja na mchezo wa pili uliochezwa Dar.

Taarifa iliyotolewa na CAF leo imeeleza kuwa kwenye mchezo wa RS Berkane dhidi ya Simba uliochezwa Februari 27, 2022 CAF imewapiga RS Berkane faini ya dola za Kimarekani 8,000 baada ya mashabiki wa timu kufanya vurugu na kutupa vitu kwenye eneo la kuchezea (pitch).

 

Pia katika mchezo wa pili uliochezwa Uwanja wa Mkapa, (Simba 1-0 RS Berkane) kiongozi wa RS Berkane Majid Madrane aliingia kwenye sehemu ya kuchezea na kuwashawishi wachezaji pamoja na benchi la ufundi kuungana naye kupinga maamuzi ya mwamuzi, jambo lililosababisha mchezo kusimama kwa muda wa dakika 5.

 

CAF imemsimamisha Madrane kutojihusisha na masuala ya michezo yanayoyohusiana na CAF kwa muda wa miezi 12 na Klabu ya RS Berkane imepigwa faini ya Dola za Kimarekani 100,000 kutokana na kitendo cha Madrane.

Leave A Reply