The House of Favourite Newspapers

Jaden Afurahia Kofi la Baba Yake

0

Licha ya Will Smith kuomba radhi kwa tukio alilolifanya la kumpiga kofi mchekeshaji maarafu nchini Marekani, Chris Rock, mwanaye Jaden Smith ’23’ ameonyesha kufurahia kitendo cha baba yake kumzaba kofi mchekeshaji huyo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Jaden ameandika: “And That’s How We Do It“ akimaanisha ‘Na hivi ndivyo tunavyofanyaga’.

Tweet hiyo imezua mjadala mkubwa kwenye mitandao, wengine wakimuunga mkono Jaden na wengine wakimpomda kwa alichokiandika. Je, ni yapo mawazo yako juu ya sakata hili?

Leave A Reply