The House of Favourite Newspapers

Ruby: 2018 Naanza Rasmi Kupambana!

BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu, sexy lady kunako Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ amefunguka kuwa, katika mwaka ujao wa 2018 amejipanga kupambana katika gemu.

Ruby alisema kuwa, alikuwa kimya kwa sababu ya kujipanga na mwakani ndiyo ataanza rasmi mapambano ya kimuziki.

“Sijatoa ngoma kwa muda mrefu, lakini mwakani (2018) mashabiki wangu wategemee mambo mazuri sana, kwani ndiyo rasmi nitajikita kwenye gemu maana nilikuwa ninajipanga,” alisema.

 Gabriel Ng’osha | IJUMAA WIKIENDA

Comments are closed.