The House of Favourite Newspapers

Hivi Ndivyo Jamal Malinzi Atakavyoondoka Kwenye Urais wa TFF

0

 

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wamenyimwa dhamana na kupelekwa mahabusu hadi Julai 3 mwaka huu kesi yao itakapoendelea tena.

Viongozi hao wangazi za juu wamepelekwa mahabusu baada ya kusomewa mashtaka 28 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam walipofikishwa leo baada ya kuhojiwa na kuwekwa chini ya ulinzi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

 

 

Wakiwa mahamani mapema leo, watuhumiwa hao walisomewa mashtaka 28 ya kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF iliyopo katika Benki ya Stanbic, Dar es Salaam.

Akitoa uamuzi huo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Wilbord Mashauri amesema kwamba watuhumiwa hao hawatopewa dhamana hadi atakapoamua kuhusu suala hilo kufuatia mabishano ya kisheria ya mawakili wa utetezi dhidi ya mawakili wa upande wa Serikali.

 

 

Mashtaka 25 kati ya 28 yaliyosomwa mahakamani hapo yanamhusu Jamal Malinzi ambapo anadaiwa kughushi michakato mbalimbali ya kifedha huku matatu yaliyobaki yakiwahusu watuhumiwa wote wawili.

Endapo mahakama itashikilia msimamo wake wa kuwaweka viongozi hao mahabusu hadi Julai 3 mwaka huu, ni dhahiri kuwa Malinzi hatoweza tena kutetea kiti cha urais wa TFF katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu. Hii inatokana na sababu kuwa, hatoweza kushiriki zoezi la usajili wa wagombea lililoanza jana na linatarajiwa kumalizika keshokutwa Jumamosi Juli 1 jioni

 

 

Wengine waliosalia katika nafasi hiyo wakigombea urais wa TFF ni Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Fredrick Mwakalebela, John Kijumbe, Shija Richard, Ally Mayay na Emmanuel Kimbe, baada ya mgombea mmoja, Athumani Nyamlani aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa TFF kujitoa.

Leave A Reply