The House of Favourite Newspapers

Saa 72 Kabla ya Kifo… Ude Ude Alipanga ‘Kuokoka’

0

 ude ude na Iq

Hamid Afidh ‘Ude Ude’ na mwenzake Abdulrauf Iqbar ‘Iqu Junior’.

Makala: Boniphace Ngumije

MWANDISHI wa Vitabu na mhamasishaji wa masuala ya ujasiriamali kutoka Afrika Kusini, Gayton McKenzie aliwahi kusema kifo hutegemewa na wachache, huchukiwa na wengi lakini ni mwisho wa kila mmoja hata kwa wasiopenda, kila mmoja wetu ataiacha dunia kwa wakati wake na njia yake.

Hivi karibuni Tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva imepata pigo baada ya kuondokewa na mtunzi mahiri na mwimbaji wa Bongo Fleva, Hamid Afidh ‘Ude Ude’ na mwenzake Abdulrauf Iqbar ‘Iqu Junior’ kwa kupigwa risasi mkoani Tanga baada ya kudaiwa kuwa ni majambazi.

Taarifa kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga, zimethibitisha kuwa Ude Ude na mwenzake walikutwa na umauti baada ya kupatikana na hatia ya wizi kwenye gari lililokuwa limeegeshwa katika halmashauri ya jiji hilo.

Ude Ude

Hamid Afidh ‘Ude Ude’.

Kuhusu Ude Ude

Marehemu Ude Ude ambaye amezikwa Jumatano iliyopita kwenye Makaburi ya Mwangazija, Kisutu Dar ameacha mke na mtoto mmoja.

Ude Ude alikuwa ni moja ya vichwa muhimu kwenye Muziki wa Bongo Fleva, amefanya kazi na wasanii wengi lakini pia amewatungia nyimbo baadhi yao  ambazo nyingi zilifanya vizuri kwenye tasnia ya muziki huo.

Moja ya kazi zake alizotunga ni pamoja na wimbo wa Lady Jaydee uitwao Wangu, wimbo ambao miaka michache iliyopita ulikuwa wa ‘taifa’.

Mbali na wimbo huo, Ude Ude ametunga nyimbo nyingine zikiwemo Si Mzima wa Ali Kiba, Oyoyo wa Bob Junior pamoja na asilimia 90 ya nyimbo za Queen Darleen ukiwemo Maneno Maneno.

Mkali huyu ambaye ameondoka bado tasnia ya muziki ikimhitaji, kabla ya kifo chake aliwahi pia kufanya kazi na mwanamitindo mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo  kwa kumtungia wimbo uitwao Leoleo pia alitunga wimbo uitwao Sababu za Urofa wa Top C.

bob_junior_sharobaro2

Bob Junior amzungumzia

Bob Junior ambaye ndiye msanii aliyefanya kazi na marehemu Ude Ude kwa muda mrefu amesema kuwa  mshikaji huyo alikuwa ni msaada mkubwa katika gemu la Muziki wa Bongo Fleva na alikuwa na malengo makubwa sana katika kazi yake ya muziki.

Showbiz: Katika kipindi chote mlichokaa pamoja uliwahi kufahamu kuwa anajihusisha na ishu za ujambazi?

Bob Junior: Hapana. Yaani hata siku moja,  nilimfahamu kama mtu wa kujichanganya na kukomaa kivyake lakini sikuwahi kufahamu kabisa juu ya hilo.

Showbiz: Mara ya mwisho mlionana lini?

Bob Junior: Siku chache tu kabla ya kifo chake, haziwezi kuzidi tatu.

Saa 72 kabla ya kifo alipanga ‘kuokoka’

Kwa upande wa Msanii wa Hip Hop, Bonge la Nyau  anayetamba na Wimbo wa Aza anasema siku tatu kabla ya kifo cha Ude Ude walikuwa studio kwa Prodyuza Alo Naim wakirekodi wimbo wake.

Showbiz: Katika siku hiyo ya mwisho uliyokuwa naye kipi ambacho unaweza kumzungumzia?

Bonge la Nyau: Ninaweza kusema ni kama jamaa alikuwa anaokoka kwa ajili ya gemu la muziki. Unajua huko nyuma hakuwa siriasi kufanya muziki, lakini siku hiyo alikuwa anazungumzia muziki tu wakati wote na alikuwa anasisitiza kuwa wimbo huo ukitoka ambao tulikuwa bado hatujaupa jina ndiyo alikuwa ameingia rasmi kwenye muziki, yaani kwa kuwekeza nguvu zote katika muziki.

Lakini malengo yake hayo hayakuweza kutimia, amekufa mapema aisee kifo ni kitu kingine kabisa haijalishi jamaa amekufaje lakini inauma sana.

Binti wa Miaka 19 Aliye Tembea na Wake za Watu Ndiye Huyu Hapa-Part I

PT 2- Binti wa Miaka 19 Aliye Tembea na Wake za Watu Ndiye Huyu Hapa-Part I

Mzungu Dar Afumwa Live Akilawitiwa na Vijana 3, O.F.M Yanyaka Tukio Zima

Leave A Reply