The House of Favourite Newspapers

SABABU YA VEE MONEY KUZUNGUKA NA JUX

Vanessa Mdee ‘Vee Money’ na Juma Khalid ‘Jux’

IKIWA imepita wiki moja tangu wamalize ziara yao ya In Love and Money, staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amefunguka sababu ya kuzunguka mikoani na Juma Khalid ‘Jux’ kuwa ni mashabiki watambue mbali na muziki wao ni wapenzi.

Akichonga na Star Showbiz, Vee Money alisema kwamba, Jux anamsapoti sana kimuziki pamoja na kuwa ni wapenzi na ndiyo sababu iliyochangia kumchagua yeye tu na si mwingine.

“Nilifanya hii ziara na Juma (Jux) kwa sababu sisi ni wapenzi kuna wengine wanasimama na kitu kimoja tu cha kimahusiano lakini sisi tumeonesha pamoja na kuwa wapenzi tunaweza kufanya muziki pia wa pamoja na jamii ikafurahia kuona kile ambacho tumekifanya katika mikoa mbalimbali ya Tanzania na ninaamini muziki wetu kwa sasa umekuwa na upo mpaka nje ya Tanzania,” alisema Vee Money.

Comments are closed.