The House of Favourite Newspapers

Sabaya Atua Mahakamani na Jezi ya Wananchi – Video

0

ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kusikiliza kesi inayowakabili.

 

Sabaya akiwa amevaa jezi ya timu ya Wananchi Yanga na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo leo Ijumaa Septemba 24, 2021 wakikabiliwa na mashtaka matano katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27 ya mwaka 2021 ikiwemo kosa la utakatishaji fedha Sh 90 milioni.

 

Itakubukwa kuwa Klabu ya Yanga itachuana na mwamba wa soka Tanzania, Wekundu wa Msimbazi, Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii hapo kesho.

Sabaya na wenzake sita wapo mahakani kuendelea kusikiliza ushahidi wa upande wa Jamhuri ulioanza Alhamisi chini ya Hakimu Patricia Kisinda.

Leave A Reply