Safari ya Kwanza ya Air Tanzania kutoka DAR – MUMBAI Yazinduliwa

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,  Isaack Kamwelwe (wa tatu kushoto) akikata utepe wakati wa hafla fupi ya uzinduzi rasmi wa safari ya kwenda Mumbai nchini India kwa ndege ya Air Tanzania (ATCL) ikiwa ni ya kwanza kwa shirika hilo kutoka nje ya Bara la Afrika na ni safari ya moja kwa moja kutokea Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Ndege  hiyo imeondoka jana , Julai 17, 2019.

…Akikata keki wakati wa uzinduzi rasmi wa safari ya ATCL kwenda  Mumbai.

 

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe,  jana, Jumatato, Julai 17, 2019,  amezindua safari ya kwanza ya kimataifa ya Shirika la Ndege nchini (ATCL) ya kutoka  Dar es Salaam kwenda Mumbai,  India.

Kamwelwe amezindua safari hiyo, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwenye jengo jipya la safari za kimataifa ‘Terminal 3’ ambalo linatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.

Katika hafla hiyo, amewapongeza Watanzania wote ambao wamekuwa waaminifu kwa kulipa kodi kwa serikali, akisema ndiyo waliowezesha ununuzi wa ndege sita za shirika hilo na ujenzi wa jengo hilo jipya.

“Ni jitihada zenu kwenye ulipaji kodi ndizo zimewezesha kufikia mafaniko haya makubwa pamoja na mengine mengi yanayokuja, ni lazima mjipongeze,” ameeleza.

Ameongeza kuwa safari za kimataifa zitasaidia katika kukuza biashara na uwekezaji nchini, kuongeza shughuli za utalii, kuunganisha nchi na wananchi wake na mataifa mengine duniani, kukuza uchumi na kuboresha maisha ya Watanzania.

 

Loading...

Toa comment