The House of Favourite Newspapers

SAID KATAMBO WA LINDI AIBUKA MSHINDI WA PIKIPIKI DROO YA SABA -VIDEO

Droo ya saba ya Shindano la Tusua Maisha na Global, imechezeshwa Jumanne ya Agosti 7, 2018, saa kumi jioni mubashara kupitia Global TV Online ambapo msomaji Said Katambo wa Nachingwea, Lindi ameibuka mshindi wa pikipiki mpya.

 

Mbali na Said, wengine waliong’ara ni Boniface Malick wa Bunju A jijini Dar es Salaam aliyejishindia dinner set, Benard Kasembe wa Pugu Mwakanga aliyejishindia head phones za kisasa za Beats by Dre na Ally Bakari, Mkazi wa Vikindu aliyejishindia jezi mpya.

 

Wiki iliyopita, ilikuwa ni zamu ya Erasto Luponelo, mkazi wa Makambako mkoani Njombe ambaye aliibuka mshindi wa pikipiki, na kuungana na wenzake watano waliotangulia ambao mpaka sasa wameshajishindia pikipiki.

 

Mbali na Erasto, washindi wengine katika droo hiyo ya sita walikuwa ni Victor Lucas wa Tanga aliyejishindia jezi orijino ya timu mojawapo ya Uingereza, Erasto Omary wa Boko jijini Dar aliyejishindia Headphone za kisasa za Beats by Dre na Augustine Haule wa Kinyerezi jijini Dar aliyejishindia dinner set.

 

Kabla ya droo hiyo ya sita, katika droo ya tano, Emanuel Tenga wa Moshi, Kilimanjaro aliibuka mshindi wa pikipiki huku Catherine Tuli wa Mbagala jijini Dar es Salaam akijishindia dinner set, Pantaleo Asenga wa Manzese akijishindia Headphone za kisasa za Beats by Dre na Malugu Menya wa Mererani akiondoka na jezi.

 

“Washindi wote wa droo ya tano na sita, wanatarajiwa kukabidhiwa zawadi zao Ijumaa, wale wa mikoani wawaandae wawakilishi wao kuja kuwapokelea zawadi zao na kwa wasomaji wengine, nawasihi waendelee kushiriki shindano hili.

 

“Kutakuwa na jumla ya droo kumi na mbili kwa hiyo nafasi za kushinda bado ziko nyingi na lengo letu ni kurudisha fadhila kwa wasomaji wetu,” alisema Abdallah Mrisho, Meneja wa Global Publishers.

 

Ili kuwa miongoni mwa washindi, nunua gazeti lolote linalochapishwa na Global Publishers kati ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra kisha funua ukurasa wa pili ambapo utakutana na kuponi yenye maelekezo ya namna ya kushiriki.

 

Itume namba maalumu inayoonekana juu ya kuponi kwa njia ya meseji kwenda namba 0719386533. Hakikisha unahifadhi kuponi au gazeti lako kwani linahitajika wakati wa kuchukulia zawadi vigezo na masharti vinazigatiwa.

Comments are closed.