The House of Favourite Newspapers

Said Ndemla yamkuta Simba

KIUNGO mwenye zali la kupendwa na mashabiki wa Simba, Said Ndemla anadodea benchi. Amekata tamaa ya kuvaa uzi wa kikosi cha kwanza msimu huu.

 

Rekodi zinaonyesha kuwa Ndemla mara ya mwisho kupata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza ilikuwa Mei 8 katika mchezo dhidi ya Coastal Union msimu uliopita.

 

Ambapo tangu apate nafasi amekosa michezo saba ya mwisho ya ligi msimu ulioisha pamoja na miwili ya mwanzo msimu huu, akikosa hata nafasi ya kuwa mchezaji wa akiba. Jumla anakuwa amekosa michezo tisa ambazo ni sawa na dakika 810 za uwanjani.

 

Ukiachana na ligi kuu, mara ya mwisho Ndemla kupata nafasi ya kucheza ilikuwa katika michezo miwili ule dhidi ya Sevilla na Gwambina FC ambapo alifunga bao la kusawazisha.

 

Hali inazidi kuwa ngumu kwa mchezaji huyo kutokana na uwepo wa viungo wengine kama Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Sharaff Shiboub, Mzamiru Yassin, Clatous Chama, Gerson Fraga na Francis Kahata ambao wote wameshapata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha Simba.

 

 

“Nafasi yangu naiona finyu sana msimu huu haswa baada ya timu kuondolewa kwenye mashindano ya kimataifa, kwa vile kule wangecheza wengine na sisi tungetamba huku, lakini mambo yamegeuka,” aliongeza mchezaji huyo aliyewaringia Yanga na kusaini Simba.

Comments are closed.