The House of Favourite Newspapers

Saido Ntibazonkiza Kukiwasha Dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa, Dar

0

KOCHA Mkuu wa Simba, Juma Mgunda ameweka wazi huenda akamtumia mchezaji wake mpya, Saido Ntibazonkiza katika mchezo wa leo Ijumaa dhidi ya Tanzania Prisons.

Mbali na kutumia staa huyo wa zamani wa Yanga, Mgunda ameweka wazi kuwa kikosi chake kiko vizuri kuhakikisha kinapata alama tatu dhidi ya Wajelajela hao kutoka Mbeya.

Prisons imeahidiwa dau la Sh milioni 30 kutoka kwa wadhamini wao ikiwa wataifunga Simba leo.

Simba leo Ijumaa wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Tanzania Prisons katika mchezo unaotarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Kocha Mgunda alisema kuwa huenda akamtumia Saido mchezaji huyo kutokana na kuwa tayari kwa ajili ya mchezo huo huku akikiri kuwa mchezo kati ya na Prisons huwa mgumu lakini malengo yao ni kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.

“Saido ni mchezaji wetu na yupo tayari kwaajili ya mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prison, tayari ni mchezaji ambaye ameshasajiliwa na Simba na kazi yake kubwa mpaka akasajiliwa ni kuitumikia Simba hivyo kama huenda nikamtumia kesho (leo).

“Tanzania Prisons mara zote imekuwa ni timu ngumu na mechi yetu dhidi yao huwa na ushindani mkubwa hivyo kwetu tayari tumeshajiandaa kwa ajili ya kuitafuta matokeo yalikuwa mazuri,” alisema kocha huyo.

Na Marco Mzumbe

Leave A Reply