The House of Favourite Newspapers

Sakata la Tanga Cement Kuuzwa, Chama Cha Walaji Chadai Hakikushirikishwa

Wadai Waziri Amedanganya, Wakili Afunguka Uhalali Kampuni ya Chalinze

0

 

MKURUGENZI wa Chama cha Walaji Tanzania,Bernad Kihiyo, amesema kauli iliyotolewa bungeni kuwa wadau wote walishirikishwa na kuridhia suala la kuunganisha makampuni ya Tanga Sementi na Twiga Sementi,imelenga kuficha ukweli kwa kuwa wo kama wadau hawajawahi kushirikishwa katika hatua hiyo.

Amesema kwa sasa wanachoona ni mazingira ya Kampuni ya Saruji ya Tanga kutka kubaki peke yake katika soko la Saruji hali itakayowafanya walaji wasiwe na chagua zaidi ya kununua bidhaa hiyo kwa gharama za mzalishaji huyo.

Kihiyo,alitoa kauli hiyo jana jijini Dar esSalaam,alipoongea na waandishi wa habari na kueleza kuwa wao kama watetezi wa waliingia katika kesi hiyo ya kupinga kuunganishwa kwa kiwanda cha Tanga Sementi na Twiga Sementi kwa lengo la kulinda maslahi ya walaji.

“Kauli kuwa wadau wote tulishirikishwa kwenye uamuzi wa kuunganisha Twig na Tanga Sementi,wahusika hawakumuambia ukweli Waziri,mimi kwa nafasi yangu ya Ukurugenzi wa chama cha kutetea walaji ninaeleza wazi hatukushirikishwa katika hili”alisema Kihiyo.

 

 

Aliongeza kuwa dhamira yao ni kuona mlaji haumizi na ushindani wowote wa kibiashara kwa badhi yao kuhodhi soko kwa njia zisizo halali ikiwemo kuhodhi nguvu ya kuzalisha bidhaa na kuua viwanda vingine.

“Katika jicho la Mbali tunaweza kuona kuwa mzalishaji anaweza akashusha bei, lakini niwaambie wafanyabiashara wanatabia ya kulana na hii anaweza hta kushusha bei kwa muda kwa ajili ya kuwaondoa wengine sokoni na akibaki peke yake anapandisha bei huku wale wazalishaji wadogo wakiwa wameshafunga biashara zao”alisema

Kwa Upande wake Wakili Melchisedeki Lutema alisema Umauzi wa nMhakama ya Kibiashara ya tarehe 23 Sept 2022, juu ya kuungana au kutokuungana kwa makampuni ya Twiga na Tanga Sementi yalieleza wazi kuwa yamezuia kuungana kwa makampuni hayo na hayakutoa muda maalum wa kuisha kwa uamuzi huo.

 

Aliongeza kuwa katika mazingira hayo kama kuna mtu au taasisi iliona haijatendewa haki ilipaswa kuomba marejeo ya shauri hilo tofauti na ilivyofanywa na Tume ya Ushindani ya kuruhusu muungano bila kujali uamuzi wa kimahakama

Akizungumzia kufutwa kwa kampuni ya Chalinze Sementi, wakili huyo alieleza kuwa wameshangazwa na utaratibu uliotumika kwa kuwa wateja wake hawakupewz taarifa na sababu za kufutwa kwake

“Chalinze ni kampuni iliyosajiliwa 2021 na inatambulikana serikali ndiyo maana hat kwenye rufaa yetu iliunganishwa kwa kuwa Sheria inasema kama yamefanyika maamuzi ambayo mtu anaona kisheria yanaweza kuingilia maslahi yake anaweza kulalmika na Chalinze ni mmoja wa watu waliooona maslahi yake yanaweza kuingiliwa ndiyo akalalmika na anaweza kulalamika na haijalishi kama ameanza kuzalisha au au laa”alisema Wakili Lutema

Leave A Reply