The House of Favourite Newspapers

Sakata la Waraka wa KKKT, Mwigulu Amsimamisha Kazi Msajili wa Vyama – Video

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.

 

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba, kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa kwa maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania.

 

Mwigulu amesema Waraka wa barua unaodaiwa kuandikwa na Serikali dhidi ya Makanisa unaosambaa mitandaoni si wa kweli na kwamba ni uhalifu umefanywa na watu wasioitakia nchi mema na kwamba Serikali haipingani na dhehebu lolote na pale ambapo kuna uhitaji wa kufanyia kazi jambo kuhusu taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo taratibu huwa zinatumika kuzungumza na sio kama ilivyofanywa taarifa hiyo inayosambaa.

 

“Serikali inalinda uhuru wa kuabudu na waumini hivyo taarifa hiyo inayosambaa ni batili na tayari uchunguzi umeanza kufanyika. Tunawaomba viongozi wa dini waendelee na kazi zao, nasema jamii iwe macho na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya jamii na wasifanyie kazi taarifa hizo,” amesema Mwigulu.

 

Dk Nchemba amesema amefuatilia barua hizo na kuona zina mkanganyiko wa anuani.

 

Video: Waraka wa KKKT, Mwigulu Amsimamisha Kazi Msajili wa Vyama

Comments are closed.