MAAJABU! Samaki mkubwa aina ya Chongoe ambaye ni jamii ya nyangumi, hivi karibuni alionekana kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi, Mbezi jijini Dar es Salaam na kuzua taharuki kubwa kwa wavuvi na mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, samaki huyo ambaye anaelezwa kuwa bado ni mtoto, alikufa na kusukumwa na mawimbi ya bahari mpaka ufukweni mwa bahari ya Hindi. Vijana kadhaa walionekana wakichangamkia dili kwa kumpasua samaki huyo na kuchukua mafuta yake, kwa ajili ya matumizi ambayo bado hayajafahamika.
Mpaka kamera zetu zinaondoka ufukweni hapo, bado vijana hao walikuwa wakiendelea kumpasua samaki huyo huku watu mbalimbali wakikusanyika, kumshangaa na kupiga picha na samaki huyo.
Samaki kama huyo, akiwa na urefu wa takribani futi 40, alionekana mwaka 2016 akiwa amekufa, kwenye Pwani ya Masoko, Kilwa mkoani Lindi.
TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILO