The House of Favourite Newspapers

Samatta, Juzi, Jana na Leo, Anaendelea Kuwanyoosha Ubelgiji, Apachika Bao Genk Ikiitwanga Kortrijk

samatta-bao-europaatMshambuliaji Mbwana Samatta wa Genk kutupia mabao hii ikiwa ni mechi ya pili mfululizo.
Samatta amefunga bao la pili katika dakika ya 42 wakati timu yake ya KRC Genk ikiitwanga Kortrijk kwa mabao 3-0 katika mchezo wa mchuano wa Ligi ya Ubelgiji.
Alejandro Pozuelo yeye alifunga bao katika dakika ya 68 kuhitimisha ushindi huo mnono wa Genk ikiwa nyumbani.
Mechi iliyopita Genk ikivaa Eupen, Samatta alifunga bao pekee na timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0. 

Comments are closed.