The House of Favourite Newspapers

Samatta Kusepa Uingereza – Video

Ameelezea namna ambavyo aliamua kuondoka TP Mazembe na kwenda kujiunga katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji ambapo mwanzoni hakuaminiwa alipojiunga nayo.

 

Samatta amesema wakati anajiunga na timu hiyo alionekana mchezaji wa kawaida licha ya kuwa aliondoka TP Mazembe akiwa staa lakini kubwa zaidi akiwa ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika.

 

Akizungumza katika kipindi cha Kick Off ya 255 Global Radio Samatta alisema alivyojiunga na KRC Genk alipelekwa katika kikosi cha timu B ambacho kilikuwa kinashiriki ligi yake, lakini baadaye akaanza kufunga mabao na ndipo walimpandisha kucheza kwenda timu A.

 

“Haikuwa rahisi kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza kwa sababu wakati najiunga na Genk nilionekana kuwa nina kipaji lakini bado nilikuwa nina mapungufu fulani likiwemo suala ka kukosa nguvu zaidi ya kupambana uwanjani.

“Nashukuru Mungu kuwa nilijitahidi kupambana na kufanikwa kuwa mshambuliaji tegemeo na hadi kufikia leo nimeisaidia timu yangu kuwa mabingwa wa Ubelgiji na kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya,” amesema Samatta.

 

Amezungumzia pia kuhusu  tetesi za kuihama Genk kwenda katika ligi za Uingereza na Hispania, ambapo alisema; “Kusema kweli hizo taarifa hata mimi nilikuwa nazisikia ingawa kuna ofa zingine zilikuwa zinatajwa lakini zilikuwa hazifiki mwisho.”

 

Comments are closed.