The House of Favourite Newspapers

Samatta Atupia Mbili Genk, Ampa ‘Tabu Sana’ Kipa Karius – Pichaz

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa kuamkia leo amepachika mabao mawili kwenye mchezo wa Europa League akiisaidia timu yake ya KRC Genk kuibuka na ushindi wa mabao 4 – 2 dhidi ya Besiktas.

 

Samatta alifunga mabao yake dakika ya 23 na 69 huku akitoa assist moja katika ushindi huo ambapo Genk walikuwa ugenini ambapo timu hiyo sasa inaongoza kundi wakiwa na alama 6 baada ya kushinda michezo miwili na kupoteza mmoja. Kufikia sasa Genk imefunga mabao 7 na kuruhusu matano.

Samatta amecheza mechi 8 za Europa na kufunga mabao 9 (hatua ya makundi na kufuzu) ambapo katika hatua ya Makundi Samatta ana mabao matatu kwenye mechi 3. Hadi Samatta amehusika katika magoli 11 katika michezo 8 (Mabao 9 na asisst 2).

 

Takwimu za Jumla za Samatta msimu huu amehusika magoli 18 kwenye michezo 18. (Mabao 16 na assists 2) ambapo mpaka sasa Samatta amehusika mabao 63 katika michezo 130, (Mabao 50 na Asissts 13).

Sasa Samatta ni miongoni mwa wafungaji waliowahi kufikisha mabao 50 ndani ya klabu ya Genk. Mbwana Samatta ndiye mfungaji bora namba 6 wa klabu ya Genk Mbwana Samatta ndiye mfungaji bora wa Genk kutoka Bara la Afrika.

Comments are closed.