The House of Favourite Newspapers

Samia Kuzindua Mkutano wa Wasindika Vyakula Nchini

1-001

CHAMA cha wasindikaji  wa vyakula nchini  (Tanzania Food Processors Association  – TAFOPA) kinatarajiwa kufanya mkutano wake wa wadau wa uwekezaji wa viwanda vya usindikaji wa vyakula utakaofunguliwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Desemba 3 mwaka huu.

2-001Kutoka kushoto ni Mtaalam Mshauri wa TAFOPA, Gloria Kavishe, Mwenyekiti Suzzy Laiser na Makamu Mwenyekiti wa TAFOPA, Janet Mkony.

Mwenyekiti wa TAFOPA, Suzzy Laiser, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam  alipokuwa akizungumza na wanahabari  kwamba  mkutano huo  utaleta pamoja zaidi ya wadau 100 wakiwemo mawaziri na wakurugenzi wa idara mbalimbali za serikali na taasisi binafsi.

3-001Baadhi ya wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Amesema  lengo la mkutano huo ni kuzindua uanzishwaji na uendelezaji wa maeneo ya viwanda vya usindikaji ili kuhamasisha na kutafuta washirika kutoka mashirika ya kimataifa ambapo pia watajadili mambo mbalimbali yakiwemo kuunda timu ya wataalamu wa kukusanya takwimu na kuandaa andiko la mpango wa kutafuta raslimali.

Na Denis Mtima/GPL

Comments are closed.