The House of Favourite Newspapers

Samia Mgeni Rasmi Tamasha la Changia Damu

0

samiaMakamu wa Rais, Samia Saluhu Hassan.

Na Mwandishi Wetu

Makamu wa Rais, Samia Saluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Changia Damu, Okoa Maisha linalotarajiwa kuanza kesho katika Uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam ambako pia kutakuwa na wasanii mbalimbali.

Akizungumza na gazeti hili, Afisa Uhusiano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Eligeisha alisema Makamu wa Rais, Samia atashiriki kutoa damu Ijumaa, Februari 26, mwaka huu jijini Dar pamoja na viongozi wengine.

“Lengo la tamasha hilo linaloitwa Changia Damu Okoa Maisha ni kukusanya lita kati ya 5,000 na 6,000 ambazo ni asilimia 75 ya mahitaji ya damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.”

Alisema tamasha hilo kama linavyojieleza, kwamba wachangiaji wa damu watakuwa wanafanya hivyo ili damu hiyo ipelekwe benki ya damu kwa ajili ya wagonjwa watakaohitaji.

Katika tamasha hilo, kutakuwepo wasanii mbalimbali watakaotumbuiza bure wakiwemo vijana wa Yamoto Band na THT ambao watafanya vitu vyao wakati zoezi hilo likiendelea.

Tamasha hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Global Publishers, Clouds FM, Pepsi Tanzania, Startimes, Abbott Fund, Benki ya CRDB pamoja na Motsun Group Tanzania Ltd.

Leave A Reply