The House of Favourite Newspapers

Castle Lager Yamleta Samuel Eto’o Tanzania

 

Samuel Eto’o Fils

KAMPUNI  ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Castle Lager imemualika mmoja ya wachezaji bora barani Afrika, Samuel Eto’o Fils,  kuzindua mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira aina ya 5-A-Side utakaojengwa Oyster Bay, Dar es Salaam. Uwanja huo baada ya kukamilika utakuwa wazi kwa wananchi kucheza.

 

Nyota huyo ambaye kwa sasa anasakata kabumbu huko QATAR anatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam kesho saa tisa na nusu mchana na kupokewa na mwenyeji wake TBL kupitia Bia yake ya Castle Lager.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli, alisema  nyota huyo atashiriki katika uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa uwanja maalumu wa soka linaloshirikisha wachezaji kumi (watano kila upande) maarufu kama ‘5-A-Side soccer’ katika eneo la Oyster Bay mkabala na jengo la Coco Plaza, jirani na ufukwe wa Coco.

 

Alisema, TBL kupitia bia yake ya Castle Lager imeamua kujenga uwanja huo kama sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamiii ya Watanzania ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikiwaunga mkono kibiashara.

 

Pia amesema lengo la kumleta mchezaji huyo nchini ni kuongeza  hamasa kwa wanamichezo wenye vipaji kujitokeza kushiriki katika soka na kutoa fursa kwa Watanzania ambao hawajawahi kumuona.

Akizungumza katika hafla hiyo, mchezaji mkongwe wa soka nchini, Ivo Mapunda, ambaye pia ni balozi wa Castle Lager, alisema  anaamini uwepo wa Eto’o nchini utakuwa chachu kwa Watanzania kushiriki katika mchezo huo.

 

Kwa upande wao, wasemaji wa Simba na Yanga wamewapongeza Castle Lager kwa kusapoti maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.

VIDEO: FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.