The House of Favourite Newspapers

Sanchez anazungumza na wachezaji watatu tu United

IMERIPOTIWA kuwa Alexis Sanchez hana uhusiano mzuri na wachezaji wenzake, na hiyo imetajwa kuwa ni moja ya sababu zinazomfanya atake kuondoka Manchester United.

 

Imeelezwa na Gazeti la Metro kuwa, wakala wa Sanchez, Fernando Felicevich, sasa anahangaika kumtafutia dili la kutua PSG.

 

Mchile huyu ameshindwa kukidhi matarajio ya wengi Old Traff ord kufuatia uhamisho wake kutokea Arsenal Januari, mwaka huu. Sanchez, licha ya kuonekana mpweke Old Traff ord, pia inaelezwa hapendi mbinu za kocha wake, Jose Mourinho.

 

Anatajwa kuwa mchezaji anayependa kujitenga na wenzake, na muda mwingi huwa peke yake. Pia inaelezwa Sanchez huzungumza na wachezaji watatu tu ambao ni David de Gea, Juan Mata na Romelu Lukaku, tofauti na hao anapiga kimya.

MANCHESTER, England

Comments are closed.