The House of Favourite Newspapers

SANCHI AFUNGUKIA VAZI LAKE TATA LA HOSPITALI

MWANAMITINDO maarufu ndani na nje ya Bongo, Jane Ramoy ‘Sanchi’ ambaye kila kukicha anatingisha kwenye mitandao ya kijamii kutokana na mavazi yake ya nusu utupu, amefungukia vazi lake la kimitego la hospitali alilovaa na kupiga picha kisha kuitupia kwenye ukurasa wake wa Instagram.

 

Akizungumza na Risasi Jumamosi baada ya kubanwa kuhusu vazi hilo ambalo lilionekana wazi ni la kumtia majaribuni daktari wake, Sanchi alisema vazi hilo la hospitali yapo saizi moja ambayo ni lazima kila mgonjwa avae na alilovalishwa yeye halikumtosha ikabidi avae hivyohivyo.

 

“Mimi sio kwamba nilipenda lile vazi liwe hivyo lakini yote yapo saizi moja na nilivyovaa lilikuwa halinitoshi ikabidi nivae hivyohivyo maana nilikuwa sina jinsi.”

 

Alivyobanwa kwamba hakuona kuvaa vile ni kumuingiza majaribuni daktari aliyekuwa anamtibia, mdada huyo alisema: “Sidhani kama kuna daktari anaweza kuingia majaribuni kwa mgonjwa kwa sababu kila kukicha watu tofauti wanatibiwa tena wapo warembo zaidi.”

 

IMELDA MTEMA | RISASI JUMAMOSI

Comments are closed.