Sarafu ya Dhahabu Yauzwa Kwa Dola Milioni 20

Sarafu ya dhahabu iliyoundwa nchini Marekani mwaka wa 1993 imeuzwa mnadani kwa takriban dola milioni 20 ,kiasi kikubwa sana kilichowahi kulipwa kwa sarafu yoyote .

 

Sarafu hiyo inaitwa “double eagle”na iliuzwa katika mnada ulioandaliwa na Sotheby’s huko New York

Ilikuwa sarafu ya mwisho ya dhahabu kutengenezwa kwa matumizi nchini Marekani , lakini haikusambazwa kamwe wakati Rais wa wakati huo Franklin Roosevelt aliondoa Amerika kutoka matumizi ya dhahabu kama kigezo cha kulipa na kununua katika jaribio la kuinua nchi kutoka kwa hali mbaya ya uchumi .

 

Sarafu nyingi ziliharibiwa baadaye, na hata kutangazwa kuwa ni mali haramu. Sarafu hiyo ikawa mfano pekee ambao ungeweza kumilikiwa na sekta binafsi, kwani ilimilikiwa kwa muda na marehemu Mfalme Farouk wa Misri, na baadaye iliibiwa katika operesheni ya siri ya ujasusi huko New York mnamo 1996.

Mapambano ya kisheria ya miaka mitano yalifuata, ambayo yalimalizika kwa kuruhusu sarafu hiyo kumilikiwa kibinafsi

 

Mnamo 2002, sarafu hiyo iliuzwa kwa mnada na mbuni wa viatu, Stuart Weitzman, kwa $ 7.59 milioni

Kwa hivyo, sarafu hiyo iliyouzwa Jumanne kwa $ 19.51 milioni, na Stuart Weitzman, ndio pekee iliyoundwa kihalali mnamo 1933.

 

Sotheby iliita sarafu hiyo “iliyo nadra zaidi ulimwenguni”, na haikufelisha kwani ilizidi bei inayokadiriwa ya $ 10 milioni hadi $ 15 milioni

 

Pia ilivunja rekodi ya sarafu ya bei ghali zaidi ulimwenguni, ambayo iliwekwa na dola ya fedha “Floing Hair” iliyotengenezwa mnamo 1794 na kuuzwa kwa dola milioni 10 mnamo 2013. Sarafu hiyo ina sura ya mwanamke akiashiria uhuru kwenye upande mmoja, na tai wa Marekani kwa upande mwingine

 

Vitu vingine vilivyowahi kuuzwa kwa gharama ya juu

Kando na sarafu hiyo kuuzwa kwa bei ghali ,pia kuna vitu ambavyo mtu wa kawaida angeona havina thamani lakini viliuzwa kwa mamilioni ya fedha .kuanzia nguo ya kale hadi mashairi n ahata kunao wanaotoa kiasi kikubwa cha fedha kununua viti au nywele za watu mashuhuri .

Ala ya muziki ya violin ailiyochezwa katika meli ya Titanic

Moja ya hadithi za kukumbukwa kutoka kuzama kwa Titanic ni bendi ya vipande nane ambayo ilicheza hadi mwisho. Wakiongozwa na mwanamuziki Mwingereza Wallace Hartley, bendi hiyo ilicheza vyombo vyao wakati meli ilizama ndani ya maji yaliyoganda ya Bahari ya Atlantiki katika jaribio la kusaidia kutuliza abiria waliokuwa na hofu.

 

Kulingana na CNN, “Mwili wa Hartley uliripotiwa kutolewa kutoka kwa maji siku chache baada ya tukio hilo la Aprili 1912 na mkoba wa violin ukiwa bado umefungwa mgongoni mwake .” Zaidi ya karne moja baadaye, mnamo 2013, violin iliyoharibiwa ya Hartley iliuzwa kwa mnada kwa $ 1.7 milioni chini ya dakika 10. Ni chobo cha bei ghali zaidi kutoka kwa mkasa wa meli hiyo iliyoangamia.

Kiti cha J.K. Rowling

Kiti ambacho mwandishi J.K. Rowling aliketi wakati akiandika vitabu vyake viwili vya kwanza vya Harry Potter kiliuzwa kwa mnada mnamo 2016 kwa $ 394,000. Kiti hicho kilawavutia wengi na hasa mashabiki wa Harry Porter ambao walitaka sana kukinunua lakini aliyebahatika kukipata alitoa dola 394,000

Rinda jeupe la Marilyn Monroe

Lilikuwa vazi ambalo liliwaacha wengi kinywa wazi. Rinda jeupe na la kupendeza la Marilyn Monroe, ambalo alivaa katika The Seven Year Itch, iliuzwa mnamo 2011 kwa kitita cha $ 4.6 milioni.Tecno


Toa comment