The House of Favourite Newspapers

Saratani ya Shingo ya Kizazi Ilivyoleta DHana Finyu ya Ukatili wa Kijinsia

0

Saratani ya shingo ya kizazi ni mabadiliko yasiyo ya kawaida ya chembe chembe hai zilizopo kwenye shingo ya kizazi, maranyingi saratani hii ikiwa inaanza haionyeshi dalili zozote hivyo ni ngumu kwa mgonjwa kuchukua hatua yoyote juu ya ugonjwa huu.

Lakini kama ambavyo zilitokea zana finyu kuhusiana na virusi vya ukimwi kua kila muathirika anayepata virusi vya ukimwi jamii ilimuona kama amepata kwa njia ya ngono zembe bila kujali njia nyingine zinazopelekea maambukizi ya virusi vya ukimwi, ndivyo ilivyo hata kwenye kansa ya shingo ya kizazi ambayo watu wengi wanaamini inaambukizwa kwa njia ya kujamiiana na kua na wapenzi wengi la hasha! zipo njia au sababu nyingi zinazopelekea mtu kupata kansa ya shingo ya kizazi japo ngono zembe nayo ni sababu lakini isiwe ndo njia pekee ya kumkandamiza mwanamke alieathirika na ugonjwa huu kua amepata kwa njia ya ngono.

Nilipata wasaa wa kuzungumza na binti mmoja aliyejulikana kwa jina la Jesca Michael, alieleza jinsi anavyoifahamu kansa ya kizazi na kwamba aliwahi kusikia wakiongelea kua inaambukizwa kwa njia ya ngono zembe, na baada ya kuangalia kwenye mtandao alisoma njia hiyo pamoja na nyingine, lakini aliogopa kwenda kupima sababu watu wa kwanza kumtambulisha ugonjwa huo walimuambia unaambukizwa kwa ngono zembe pamoja na kua na wapenzi wengi, anaona hata kwenda kupima hospitali daktari atafikiri kua ni mshirika wa wapenzi wengi lakini laaah!

 

 

Inapaswa kueleweka kua saratani ya shingo ya kizazi ni virusi vinavyoambukizwa kwa njia nyingi mbali na njia inayojulikana ya kujamiiana, lakini kwa ambaye alikua hajui pia anapaswa kufahamu kua moja ya njia za maambukizi ya saratani ya shingo ya kizazi ni njia ya kujamiiana.

Takwimu zinaonyesha wanawake zaidi ya 300,000 wanakufa kila mwaka duniani kutokana na saratani ya shingo ya kizazi, na katika nchi ya Tanzania tu takwimu zinaonyesha kua watu 51 kwa kila watu 100,000 kwa mwaka, asilimia 90 ya maambukizi na vifo vinavyotokana na saratani ya shingo ya kizazi ni katika nchi zinazoendelea.

NJIA ZA MAAMBUKIZI YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

  • Maambukizi ya virusi vya HPV ambavyo ndio chanzo kikubwa cha saratani ya shingo ya kizazi kwa asilimia 99
  • Umri zaidi ya miaka 30
  • Kuzaa mara kwa mara
  • Upungufu wa kinga mwilini
  • Uvutaji wa sigara
  • Kupata mimba katika umri mdogo
  • kufanya ngono zembe na wanaume tofauti tofauti au mwanaume mwenye maambukizi ya HPV
  • Historia ya saratani katika familia
  • Kuanza ngono katika umri mdogo
  • Kufanya ngono na mwanaume asiyetahiriwa

DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

  • Kupata maumivu makali ya tumbo na nyonga.
  • Kupata maumivu makali wakati wa kujamiiana.
  • Kutokwa na damu ukeni baada ya kujamiiana.
  • Kutokwa majimaji ukeni kusiko kwa kawaida.
  • Kuhisi uchovu
  • kupungua uzito
  • kutokwa mkojo na kinyesi sehemu ya haja ndogo
  • Mguu kuvimba

 

 

NANI YUPO KWENYE HATARI YA MAAMBUKIZI?

Mbali na makundi tajwa ambayo yapo kwenye hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi lakini pia ugonjwa huu unaweza ukarithishwa kutokana na historia ya kwenu, hivyo unaweza kupata kwa njia ya kurithi. Makundi ambayo yapo kwenye hatari zaidi ni kama yafuatayo

1.Wanawake wanaotumia vidonge vya kupanga uzazi kwa muda mrefu.

2.wanawake wenye umri kati ya miaka 20-50.

  1. Kuzorota kwa kinga za mwili.
  2. Kubeba mimba katika umri mdogo chini ya miaka 17.
  3. Mwenye wapenzi wengi ambao anashiriki nao tendo la ndoa

JINSI YA KUITIBU SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Saratani ya shingo ya kizazi inatibiwa kulingana na hatua iliyopo, lakini kama saratani yako imesambaa sana hatua ya mwisho ni ya kuondoa kizazi, baadhi ya njia za matibabu yake ni

  • Matibabu ya kutumia dawa kali ili kuongeza muda wa kuishi
  • matibabu kwa njia ya mionzi
  • kuondolewa kwa mfuko wa mimba na viungo kama ovari na mirija ya uzazi
  • Kupata chanjo ya HPV
  • Kupima afya mara kwa mara

Saratani ya shingo ya kizazi ndio saratani inayoongoza kwa vifo vingi zaidi ya makundi mengine ya saratani, madaktari wanashauri kuwahi kwenda vituo vya afya kwa uchunguzi na matibabu kwani ikiwa kwenye hatua za awali ni rahisi kutibika lakini ikifika hatua ya mwisho matibabu yake ni magumu na itabidi mgonjwa afanyiwe upasuaji ili kutoa mfuko wa kizazi jambo ambalo litapelekea ugumba,  pia mgonjwa itakua rahisi kunyemelewa na maradhi mengine mengi na hata kumpelekea kifo, hivyo chanjo zinapatikana vituo vya afya wahi sasa kwaajili ya uchunguzi pamoka na chanjo ili uokoe maisha yako.

 

Imeandikwa na Roseline Danstan

Leave A Reply