The House of Favourite Newspapers

Saudia Yafungua Mipaka Kwa Mahujaji Waliochanja

0

SAUDIA ARABIA itaanza kuwapokea wageni waliopata chanjo ya Covid-19 katika mji mtukufu wa Kiislamu wa Makka ikiwa kama sehemu ya ibada ya umrah, ni takriban miezi 18 tangu kuifunga mipaka yake baada ya kuzuka janga la virusi vya corona.

 

Shirika la habari la Saudia limesema Wizara ya Hijja na Umrah imetangaza kuanzia kesho Jumatatu watapokea maombi ya raia na wakazi wake wanaotaka kushiriki ibada ya Umrah.

 

Lakini pia baadaye watapokea maombi kutoka mataifa mbalimbali ya nje, ruhusa hiyo hata hivyo imetolewa kwa masharti kwamba mahujaji wote wa kigeni lazima wawe wamepata chanjo inayotambuliwa na Saudi Arabia na wakubali kukaa karantini.

 

Ibada ya Umrah ambayo kwa kawaida inafanyika katika kipindi chochote cha mwaka, ilifunguliwa tena Oktoba kwa mahujaji wa ndani, baada ya kufungwa kabisa kutokana na mlipuko wa janga la virusi vya corona.

Leave A Reply