The House of Favourite Newspapers

SAUZ HAKUNA ‘KIBA WALA DIAMOND’

Cassper Nyovest.

NDANI ya Jiji la Johan-nesburg, Afrika Kusini au Sauz hali ya hewa inasoma nyuzi joto 13, baridi ni kali sana na wageni wengi kwao inakuwa shida kidogo, wengi wamevalia makoti na masweta ya kukinga baridi huku wenyeji wakiwa na nguo nyepeeesi kutokana na kuzoea mazingira.

 

Ukiachilia mbali hali ya hewa ya hapa, kikubwa ninachoambiwa kwenye burudani ya muziki katika jiji hili kuwa umegawanyika kutokana na sehemu na sehemu.

 

Ukienda Pretoria muziki kwao haupo kivile zaidi ya siasa, lakini ukienda katika majiji mengine kama vile Cape Town na Durban wana wakali wao wanaotikisa kwenye muziki tofauti na ilivyo kwa Tanzania ambapo vichwa viwili, Diamond na Ali Kiba ndivyo vinavyokubalika Tanzania nzima, ukienda Namibia nchi yenye wakazi wachache yaani milioni 2 na laki tatu kwao vichwa vya muziki vipo viwili tu nchi nzima tena vinafanya Muziki wa Hip Hop ambavyo ni The Dogg na Gazza.

Katika makala haya, mwandishi wetu ndani ya Johannesburg amekutana na wadau mbalimbali wa muziki nchini Afrika Kusini na kuzungumza mengi juu ya muziki tofauti unaofanywa na kukubalika;

Maphorisa.

DURBAN

Katika jiji hili ambalo ni la tatu kwa ukubwa nchini hapa baada ya Johannesburg na Cape Town, ukizungumzia wakali wanaotikisa katika muziki hutaambiwa Cassper Nyovest, DJ Maphorisa wala AKA, bali utaambiwa mtu mmoja ambaye ni muasisi wa Kwaito anayejulikana kama Mthokozi Khalthi a.k.a DJ Tira.

 

DJ Tira ametokea kuiteka Durban katika Kwaito na kufanya wasahau kabisa kama kuna aina nyingine ya muziki. Historia ya jamaa huyu ilianza kama masihara akitokea katika upigaji wa muziki kwenye sherehe ndogo na kubwa za watu binafsi na mashuhuri.

Ngoma yake iliyomtoa hasa ni Real Makoya na iliyofuata ilikuwa Woze Durban na ndiyo ilimpa jina la Mfalme wa Kwaito, Durban. Ngoma hiyo ya Woze Durban ni moja ya nyimbo zinazopendwa zaidi Durban ‘Wimbo wa Taifa wa Durban’ na maeneo ya jirani na jiji hilo.

 

Kwa historia ya Durban, DJ Tira ndiye mwanamuziki mzawa mwenye kukubalika kuliko mwana-muziki yeyote.

 

Kwa sasa anamiliki lebo yake ya Afrotainment huku akiwa na kundi lake la Big Nuz ambalo ni tishio kwenye Kwaito katika jiji hilo.

Kupitia lebo yake, DJ Tira ametoa sapoti kubwa kwa wanamuziki wanaokuwa kwa kasi katika jiji hilo kama vile Distruction Boyz wanaofanya muziki wenye mchanganyiko wa lugha mbili, Xhosa na Zulu uitwao Gqom.

Shekhinah Thandi Donnell ‘Shek-hinah’.

 

CAPE TOWN

Ukiingia katika jiji hili nalo ambalo ni la pili kwa ukubwa nchini hapa, katika muziki yupo mwanadada anayejulikana kama Shekhinah Thandi Donnell ‘Shek-hinah’ mzaliwa wa Durban, lakini makazi yake na muziki amejikita Cape Town.

 

Mwanadada huyu anayefanya Muziki wa Pop unaoku-balika zaidi Cape Town, ametokea kwenye mashindano ya vipaji vya kuimba Afrika Kusini ‘SA Idols 2012’ na kuingia hadi Sita Bora. Miongoni mwa ngoma anazotikisa nazo kwenye shoo zake ni Suited iliyotazamwa na watu zaidi ya milioni nne katika Mtandao wa Youtube.

Imezoeleka ikitokea shoo za msanii wa kimataifa katika jiji hili la Cape lazima Shekhinah atakuwa mpokeaji wa mgeni na shoo atapangiwa kufanya naye shoo. Ameshafanya hivyo kwa wakali kibao kama vile John Legend wa Marekani.

Kwaito Group.

JOHANNESBURG

Hili ndilo jiji linaloongoza kuwa na wanamuziki wengi huku likiwa na mchan-ganyiko wa muziki wa Afro House, Kwaito na Hip Hop.

Usikose muendelezo kesho Jumanne katika Gazeti la Uwazi kujua wanamuziki wanaotikisa katika jiji hili la Johannesburg na wametokea wapi mpaka kufanikiwa.

Comments are closed.