The House of Favourite Newspapers

SBL, Jeshi La Polisi Waelimisha Madereva Juu Ya Usalama Barabarani Kipindi Cha Sikukuu

0
Mkuu wa Masoko na Mkurugenzi wa Uvumbuzi Anitha Msangi wa Kampuniya Bia ya Serengeti (SBL) akiongea na madereva pikipiki (bodaboda) na bajaj katika mafunzo ya usalama barabarani na unywaji pombe kistarabu “DrinkIQ” yaliyoandaliwa na SBL kushirikiana na Jeshi la Polisi. Waliokonyuma ni Mwanasheria wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa dawati la usalama barabarani, Kamanda Deus Sokoni (Kushoto) na Mwakilishi kutoka chama cha Waendesha pikipiki Kijitonyama, Abdallah Omary. Mafunzo yalifanyika katika viwanja vya Kijitonyama Dar es Salaam, Ijumaa Disemba 23.

 

Disemba 23, 2022, Dar es Salaam.Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imefanya mafunzoya unywaji pombe kistarabu na uendeshaji vifaa vya moto katika kuelimisha watumiaji wa vyombo  vya moto juu ya usalama barabarani  ambapo nchi inaingia katika msimu wa sikukuu unaokuwa na shamra shamra nyingi.

 

Mafunzo hayo yamefanyika katika viwanja vya Kijitonyama jijini Dar es Salaam na kujumuisha ushiriki wa zaidi ya madereva 100 wa pikipiki,bajaji, polisi Tanzania na wafanyakazi wa SBL.

 

Takwimu zinaonyesha ajali za barabarani ni moja ya chanzo kikuu cha vifo Tanzania na barani Afrikaikiwa sababu kubwa kuwa uzembe barabarani, mwendo mkali na kuendesha vyombo vya moto wakati umelewa. Matukio haya huzidi katika msimu wa sikukuu hivyo elimu ya usalama barabarani ni muhimu kwa watumiaji wote.

Mwanasheria wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Dawati la Elimu trafiki, Kamanda Deus Sokoni, akizungumza na hadhara ya madereva wapatao 100 waliohudhuria mafunzo ya SBL Drink IQ. Kamanda alisisitiza na juu ya wajibu maalum walio nao madereva wa pikipiki na bajaj katika kuendeleza maisha ya abiria wao. Haya aliyasema katika kuhimiza kuendesha pale tu mtu anapokuwa na kiasi na si kwa ulevi.

 

Katika msimu huu, SBL na jeshi la polisi wameelimisha madereva kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama barabarani na kuacha kuendesha vyombo vya moto wakiwa wametumiwa kilevi.

 

Madereva magari, waendesha pikipiki na bajaji wameelimishwa juu ya unywaji kwa kiasi na kuaswa kuwa mabalozi wa usalama barabarani kwa wenzao na watumiaji wengine wa barabara.

Mwakilishi wa jeshi la polisi, CPL Asha Abdul akiongea na madereva pikipiki na bajaj wakati wa mafunzo ya usalama barabarani na kuendesha kwa usalama bila kunywa pombe “Drink IQ” yaliyoandaliwa na SBL na kushirikiana na jeshi la polisi.

 

Mkurugezi wa Masoko wa SBL  Anitha Msangi Rwehumbiza amesema, “Kupitia ushirikiano huu na Jeshi la Polisi Tanzania tunategemea  madereva magari na pikipiki tuliowapa mafunzo watakuwa mabalozi wazuri hasa katika kipindi hiki cha sikukuu ambapo tumewahimiza kutokunywa na kuendesha vyombo vya moto.

 

Madereva wetu wote wanajukumu la kuhakikisha abiria wao wamefika katika maeneo wanayokwenda salama.”

Wadau katika picha ya pamoja.

 

SBL ilionyesha video na kucheza vipindi vya kuelimisha kuwapa madereva elimu ya usalama barabarani. Zaidi ya hilo, SBL iliendelea kuwapa nafasi ya kuuliza maswali na kujibiwa ili kuangalia kiwango cha uelewa wao.

 

Pia, SBL imetumia nafasi hiyo kutanua wigo wake kwa umma hasa katika kufurahia bidhaa zake na kunywa kwa kiasi, kunywa maji katikati ya unywaji pombe na kuwa na dereva maalum (asiyelewa) au taxi na kutoendesha wakati wamelewa.

 

“Umma unahamasishwa kutembelea uwanja wa Drink IQ wa SBL uliopo katika mtandao unaopatikana katika vifaa vyote. Drink IQ ni mfumo wa kieletroniki unaopatikana kwa Kiswahili na Kingereza.

 

Mfumo huuu unatoa taarifa kuhusu viwango na aina ya vimiminika vilivyopo katika bidhaa za SBL, kiwango cha kuhimili pombe, mbinu za kufuatilia unywaji wa pombe, ukweli na mambo ya kuzusha yanayohusu matumizi ya pombe” Anitha aliongezea.

 

Mwanasheria wa Kikosi na Mkuu wa Dawati la Elimu Traffiki Makao Makuu, Kamanda Deus Sokoni alifurahishwa na juhudi za SBL katika kuelimisha madereva boda boda na Bajaji kuhusu usalama barabarani hasa katika kipindi hiki cha sikukuu.

 

“Niwapongeze SBL kwa jitihada hii kwa sababu inavutia na kuhusisha kila mdau. Mafunzo haya nina amini kabisa yatazuia ajali zisizokuwa na msingi na matukio mbalimbali  ya barabarani katika kipindi hichi cha siku kuu.” Alisema Kamanda.

 

KUHUSU SBL:

 

SBL iliyoanzishwa mwaka 1988 kama Associated Breweries, ni kampuni ya bia ya pili kwa ukubwa nchini Tanzania, na chapa zake za bia zimechukua nafasi ya zaidi ya 25% ya soko kwa ujazo.

SBL ina mitambo mitatu ya uendeshaji Dar es Salaam, Mwanza na Moshi.

 

Tangu kuanzishwa kwa SBL mwaka wa 2002, biashara hiyo imekuza jalada lake la chapa mwaka hadi mwaka. Upatikanaji wa hisa nyingi na EABL/Diageo mwaka 2010 umeongeza uwekezaji katika viwango vya ubora wa kimataifa na kusababisha nafasi kubwa za kazi kwa wananchi wa Tanzania.

 

Chapa nyingi za SBL zimekuwa zikipokea tuzo za kimataifa, zikiwemo Serengeti Premium Lager, Serengeti Lite, Pilsner Lager, Pilsner King, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness stout na Senator. Kampuni ya SBL pia ni nyumbani kwa vinywaji vikali vinavyojulikana duniani kama vile Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain Morgan Rum na Baileys Irish Cream.

 

Kufahamu zaidi, wasiliana na:

 

John Wanyancha

SBL Corporate Relations Director

Tel: 0692148857

Email: [email protected]

Leave A Reply