The House of Favourite Newspapers

SBL Yazindua Ripoti Ya Uendelevu ya Aina Yake

0
Kutoka kushoto, ni wawakilishi wa washirika wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Hamadi Kissiwa Meneja Kanda ya Mashariki wa Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC), Meneja Uhusiano na Serikali Neema Temba, Maxmillian Sarakikya Naibu Mkuu wa Chuo cha kilimo Kaole Wazazi, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa (SBL) John Wanyancha, Meneja Mawasiliano wa SBL Rispa Hatibu , Colleta Kyaitela Mhandisi kutoka Green Initiative na Michael Salali, Mwenyekiti kutoka Taasisi ya Foundation for Good Hope (FDH) katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Uendelevu ya kampuni mama ya SBL, East Africa Breweries Limited (EABL) uliofanyika katika kiwanda cha SBL Chang’ombe jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.

 

Desemba 16, 2022,  Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries (SBL) imezidua ripoti yake ya shughuli endelevu chini ya kampuni tanzu ya East Africa Breweries Limited (EABL) inayoonyesha mafanikio mengi katika Nyanja ya mazingira, jamii na utawala.

Kupitia mpango wake wa kijamii na kimaendeleo wa miaka kumi uitwao Society 2030: Spirit of Progress, unaoakisi mambo ya ESG katika maeneo sita ya Unywaji pombe kistaarabu, ujumuishi na utofauti, uendelevu makini, utazamaji kufanyabiashara vizuri na kaboni ya chini, SBL imedhihirisha utendaji mzuri.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) John Wanyancha (katikati), Meneja Mawasiliano wa SBL Rispa Hatibu (Kulia) na Meneja Uhusiano na Serikali Neema Temba (Kushoto) katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa ripoti ya pili ya uendelevu ya kampuni mama Africa Mashariki ya SBL, East Africa Breweries Limited (EABL) uliofanyika katika kiwanda cha SBL Chang’ombe jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.

 

Uzinduzi huo umehudhuriwa na wawakilishi kutoka mashirika na taasisi zinazoshirikiana na SBL, ikiwemo Foundation for Disabilities Hope (FDH), Green Initiativena Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC).

“SBL inajivunia kuwa mstari wa mbele katika kuchochea maendeleo endelevu kwa njia ya kibunifu na ya kipekee inayoakisi ujumuishi.

Tunategemea kuendeleza mpango huu na kutimiza malengo mengi” Alisema John Wanyancha Mkurugenzi wa Mahusiano ya Umma wa SBL.

Katika kubadilisha mitazamo ya watu kuhusu matumizi ya pombe, SBL inatumia kampeni yake ya unywaji kistaarabu, endesha kistaarabu.

 

Jifunze kuhusu pombe kupitia tovuti maalum ya DrinkiQ, SBL imewafikia zaidi ya madereva 5000 nchi nzima, imeelimisha zaidi ya wanafunzi 8,200 juu ya unywaji katika umri mdogo na kuwashawishi zaidi ya watu 2000 kujifunza kuhusu matumizi ya pombe (DrinkiQ) ndani ya mwaka 2022.

Katika Nyanja ya ujumuishi na utofauti, inayoangaliwa na serikali na sekta binafsi SBL imejikita katika kutoa ufadhili wa masomo ya kilimo kupitia programu yake ya Kilimo Viwanda, iliyofadhili zaidi ya wanafunzi 200 wanaotoka katika familia zisizo na uwezo huku wanawake na watu wenye ulemavu wakipata nafasi sawa.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Kaole Wazazi College Maxmillian Sarakikya amesema ya kwamba mchango wa SBL kwenye elimu ni muhimu“ Hii kampuni imefanya jambo kubwa sana kuinua vijana kimasomo hasa kilimo, tendo la kuigwa kama mfano na makampuni na wadau wengine wa elimu.

Zaidi ya hilo, mwakilishi kutoka FDH Michael Salali, ambaye ni Mwenyekiti wa taasisi hiyo inayoshirikiana kwa ukaribu na SBL aliongeza kwa kusema “Tunajivunia kushirikiana na SBL katika agenda ya kutanua ujumuishi na utofauti wa watu katika hilo SBL imewainua watu wenye ulemavu kwa kuwapa mafunzo ya kilimo, fedha na ujuzi”

SBL imejikita katika kuzipa jamii uhakika wa maji, katika kutimiza hilo, SBL imefanikisha kutekeleza miradi zaidi ya ishirini nchini ikiwemo mradi wake wa hivi karibuni katika kata ya Basuto, wilayani Manyara, wa tanki la kutibu maji.

Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo, mwakilishi kutoka Green Initiative Company Limited Colleta Kyaitela, aliongeza kwa kusema;

“Sasa watu wengi katika jamii zilizopata miradi hii wanafaidika na uhakika wa maji, jambo muhimu kwa maendeleo ya jamii yoyote duniani”.

Miradi ya maji ya SBL, imesaidia upatikanaji wa maji safi na salama kwa kwa watu 14,000 ndani ya kata ya Basuto, ambapo mradi unasafisha lita 900,000 za maji ndani ya masaa 12, uwezo maradufu zaidi ya hitaji la maji la eneo hilo la lita700,000.

Katika Nyanja ya mazingira SBL imepanda miti zaidi ya 5,000 wilayani Kongwa, mkoani Dodoma. Pia, imefanikiwa kuhakikisha haitupi taka katika madampo kutoka viwandani zinazosababishwa na uzalishaji.

Mwakilishi kutoka NEMC Hamadi Taimuru Kissiwa, ambaye ni Meneja Kanda ya Mashariki aliongeza katika hilo kwa kusema“ SBL inaonyesha kwa mfano ilivyo muhimu kwa wawekezaji na makampuni kufanyakazi zao kwa kuzingatia mazingira na masuala ya tabia nchi.

“Karibu asilimia mia moja ya plastiki zote katika viwanda vyetu uchakatwa na kutumiwa upya na kuozeshwa.

Hii ni ongezeko la juu zaidi ya mwaka 2022 ambapo asilimia tisini ya plastiki zetu zilichakatwa tena na zaidi ya 2022 ambapo tuliweka lengo la asilimia tisini na nane” the report stated.

Ripoti hii inaleta mjadala muhimu katika sekta binafsi na umma kwa vile maendeleo endelevu ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya karne ya ishirini namoja.

Leave A Reply